Friday 7 November 2014

KISUKARI HUSABABISHWA NA MTINDO WA MAISHA




Ugonjwa huu hutokea pale ambapo tezi ya kongosho'Pancrease'inaposhindwa kutengeneza kichocheo aina ya Insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka au kushuka kwa kiwango cha sukari damuni'hyperglycemia'.




AINA ZA KISUKARI:1-
Huwaathiri sana watoto na vijana iwapo seli aina ya beta na langerhans zinazozalisha insulin zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yoyote ile na kusababisha upungufu au ukosefu
 kabisa ya insulin kwenye damu na hapa sababu kuu ni kushambuliwa kwa tezi hii haswa na magonjwa
yanayosababisha upungufu wa kinga mwilini.

Wagonjwa wa aina hii huishi kwa sindano ya insulin maisha yao yote'Insulin Dependant Diabetes Mellitus-IDDM'.

2-Aina hii hutokea ukubwani na husababishwa na kupungua kwa ufanisi utendaji kazi wa homoni ya insulin.Unene ulopitoliza au kutokufanya mazoezi ndio visababishi vikuu kwani hapa insulin huzalishwa katika kiwango cha kutosha ila tatizo lpo kwenye wa utendaji kazi wake.

Wagonjwa hawa hawahitaji kuishi kwa sindano ya insulin.'Non Insulin Dependant Diabetes Mellitius-NIDDM' 

.3-Hutokea pale kunapotokea ongezeko ktka kiwango cha sukari ktka damu wakati wa ujauzito ingawa hupoa baada ya kujifungua..

Pili,Kisukari kutibika moja kwa moja si rahisi sana ,kwa mfano mgonjwa wa type 1 anahitaji Insulin maisha yake yote na sijasioma sehemu kuona mgonjwa wa Type 2 amepona kabisa,ila unaweza kupunguza uwezekano wa kupata madhara na ukaishi muda mrefe
Madhara ya kisukari-

Kupungukiwa nguvu za kiume
-KUTOONA VIZURI
-Vidonda kutopona haraka hasa vya miguuni
-NEURONES kuharibika na kuharibu sensations za mwili
-Matatizo katika figo

-Kupungukiwa kinga ya mwili

LISHE KWA MGONJWA WA KISUKARI



Elimu ya lishe ni muhimu sana, kwani madhara ya ugonjwa huonekana 
haraka na hata kusababisha kifo upesi, iwapo mtu ataendelea kula bila kujijua vyakula vilevile vilivyosababisha tatizo la kiafya alilonalo.
Kwa ujumla, mgonjwa wa kisukari (Diabetic), hana mipaka mingi ya vyakula, anaweza kuendelea kula vyakula vingi kama kawaida iwapo atajua jinsi ya kula, kiasi gani na kwa wakati gani. Hata hivyo, kama ulaji wake ulikuwa hauzingatii ulaji sahihi, baada ya kuugua hana hiyari bali kufuata kanuni za ulaji sahihi.

Kanuni kuu ya ulaji anayopaswa kuzingatia mgonjwa wa kisukari ni kula kiasi bila kushiba sana, kula kwa muda uleule kila siku, na kula mchanganyiko wa matunda, mboga na nafaka zisizokobolewa. Hii ina maana kwamba mgonjwa anatakiwa asisikie njaa wala shibe muda wote wa siku.

KITU GANI UNAKULA?
Bila kujali kama una kisukari au la, afya bora iko mikononi mwako kwa kuwa na hiyari ya kuchagua unachokula. Lakini unapokuwa tayari mgonjwa, unakuwa huna hiyari tena ya kuacha kuzingatia ulaji sahihi, vinginevyo unakiita kifo haraka. Kimsingi, mgonjwa wa kisukari azingatie zaidi ulaji wa vyakula vitokanavyo na mimea, aache kula vyakula vya kusindika, vyenye sukari na mafuta mengi.

WAKATI GANI WA KULA?
Suala la kujali muda wa kula kwa mgonjwa wa kisukari ni la lazima, kwa sababu atatakiwa wakati wote kudumisha kiwango cha sukari mwilini mwake kwa kula kwa wakati uleule ili kuepuka kusikia njaa ambayo husababisha sukari kushuka kwa kasi.

KIASI GANI UNAKULA?
Vilevile suala la kula kiasi kwa mgonjwa wa kisukari si la hiyari tena, bali ni la lazima. Hata mtu akila vyakula bora vyenye virutubisho vya hali ya juu kiasi gani, kama akivila kupita kiasi huweza kusababisha unene ambao ni sababu moja wapo ya ugonjwa wa kisukari, hivyo ni muhimu kuzingatia kiasi.

Mgonjwa wa kisukari hahitaji kuwa na chakula maalumu, bali anatakiwa kutilia maanani ulaji wa mboga, matunda na nafaka zisizokobolewa. Lishe ya mgonjwa wa kisukari ni ya kawaida tu yenye vyakula vyenye virutubisho vingi na mafuta kidogo na kiasi kidogo cha wanga.

ZINGATIA
Mgonjwa wa kisukari anashauriwa kula matunda, lakini anakatazwa kunywa juisi za matunda. Halikadhalika, matunda kama ‘Apples’, ‘Peas’ na mengine ya jamii hiyo, ni bora yaliwe pamoja na maganda yake. 
Miongoni mwa matunda bora kabisa kwa mgonjwa wa kisukari ni zababi mbivu, hizi zikiliwa kila siku mara tatu kwa siku, huweza kuwa tiba kabisa ya kisukari. 

Halikadhalika majani ya embe nayo ni dawa ya kisukari. Loweka majani mabichi ya mwembe, kiasi cha kiganja kimoja (gramu 15), kwenye nusu lita ya maji usiku kucha, kisha asubuhi yakamue upate maji yake, kunywa kila siku asubuhi na unaweza kukidhibiti kisukari, hasa kile kinachopanda nyakati za asubuhi.

2 comments:

ALLY SHAABAN MGIDO'S said...

HASWA LIFESTYLE TULIONAYO SASA NDIO KICHOCHEO KIKUBWA KWA MAGONJWA MENGI HIVI SASA

ALOE VERA GELLY
*pressure
*kisukari
*vidonda vya tumbo
*kuongeza nguvu
*kupunguza aleji mwilin
*kuondoa sumu mwilin
*kusafisha na kusaidia mmeng'enyo wa chakula
*uvimbe
*arthritis

Call,whatsapp kama waitaji or kujuzwa kuhuxu matatizo mbalimbali ya kiafya +255 783 149 561

ALLY SHAABAN MGIDO'S said...

Kuna watu hudhani ukiwa mnene au mwenye uzito mkubwa ndiyo kuwa na afya na ndiyo maana wengine wakikonda basi huchanganyikiwa kabisa.

Lakini uzito au unene uliozidi ni ugonjwa tena ugonjwa mubaya kabisa ambao unapaswa kuwa makini nao sana kwani ni chanzo cha magonjwa mengine mengi kama vile kisukari, kolesteroli, shinikizo la juu la damu na orodha inaendelea.

Kila mmoja anapaswa kuwa na uzito unaomstahili kulingana na urefu wake.

Na je uzito na unene kupita kiasi hutokeaje mwilini?

Mfumo mkuu wa fahamu katika ubongo hutambua kushuka kwa kiasi cha nguvu kinachopatikana kwa ajili ya matumizi yake.

Hisia za kiu au njaa pia hutokea kunapotokea kupungua kwa nguvu mwilini. Pengine ulikuwa bado hujuwi ni kwa jinsi gani njaa au kiu hutokea mwilini au ni nini kinacholeta njaa au kiu mwilini. Hivyo Hisia za kiu au njaa hutokea kunapotokea kupungua kwa nguvu mwilini.

Ili kuiamsha nguvu toka katika mafuta yaliyohifadhiwa, kunahitajika mwingilio maalumu wa ki-homoni. Zoezi hili huchukuwa muda mrefu zaidi na pengine mazoezi zaidi kwa mishipa huhitajika kuliko udharura wa uhitaji wa nguvu unavyohitajika na ubongo.

Sehemu ya mbele ya ubongo hupata nguvu ama kutoka katika nguvu inayozarishwa kwa nguvu za maji au kutoka katika sukari kwenye mzunguko wa damu. Nguvu zitokanazo na maji huhitajiwa kwa dharura zaidi siyo katika kuzarisha nguvu tu, bali hata katika mifumo yake ya usafirishaji ambayo hutegemea maji zaidi.

Kwa hiyo hisia za kiu na njaa huja kwa pamoja kuonesha mahitaji ya ubongo. Hatuzitambui hisia za kiu, na tunazichukulia hisia zote kuwa ni hitaji la kula. Tunakula chakula hata wakati mwili unapotakiwa upokee maji. Watu waliopunguza uzito wao kwa kunywa maji kabla ya kula, wamefanikiwa kuzitofautisha hisia hizi mbili. Hawakula kuzidi ya kipimo kuituliza kiu ya mwili kwa maji.

Hata hivyo, watu wengi sana kote duniani huwa hawafuatilii lolote kuhusu uzito wao. Uzito uliozidi ni ugonjwa na ni hatua ya kwanza katika kuporomoka kwa mwili wa binadamu. Kila mmoja anapaswa kujua kama uzito alionao unafaa kwa mwili wake au la.

Kwanini watu wanakula sana?:

Moja sa sababu ya kuongezeka kwa uzito au unene ni hulka ya watu kupenda kula chakula kingi na hili kwa wengine ni shida, yaani kuna mtu ukimkuta anakula chakula kilichopo kwenye sahani ni kile wanaweza kula watu wawili mpaka watatu lakini yeye anakimaliza peke yake na bado ataongeza na soda juu amalizapo hicho chakula.

Ni nini hasa kimepelekea tatizo hili la kuongezeka kwa njaa kwa baadhi ya watu?:

Ubongo wa binadamu una ukubwa kama 1/50 ya uzito wa mwili. Inasemwa, ubongo una seli neva kama tilioni 9, inasemwa, zaidi ya asilimia 85 ya seli za ubongo, ni maji.

Asilimia 20 ya damu yote mwilini imeelekezwa na inapatikana kwa ajili ya ubongo. Hii inamaanisha ubongo unahitajika kuchukua kila unachokihitaji kwa ajili ya kazi zake toka katika mzunguko wa damu.

Ubongo ni moja kati ya ogani pekee za mwili ambazo hufanya kazi muda wote hata katika usingizi mzito, huzishughurikia taarifa zote toka katika maeneo mbalimbali ya mwili na zile zinazouingia toka katika mazingira, jamii na hata zile toka mazingira ya ki-usumaku.

Katika kushughurikia kazi zote hizo, ubongo hutumia kiasi kikubwa sana cha nguvu. Wakati huo huo ubongo hutumia nguvu katika kutengeneza mahitaji ya mwanzo na jumbe kemikali (chemical messengers) ambazo zimetengenezwa toka seli za ubongo na ambazo zinatakiwa kusafirishwa kwenda miishio ya neva kuzunguka mwili.

Endelea kuisoma hii makala yote kwa kubonyeza hapa => http://goo.gl/w3MPtL

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!