Thursday, 27 November 2014
FARAJA NYALANDU KATIKA MKAKATI WA DUNIA KUWA MAHALI BORA KWA WATOTO
Huwezi kuokoa dunia katika masaa 48 lakini kama ukikusanya mawazo, mbinu na ushauri mbalimbali, unaweza kupata ufumbuzi wa muda mrefu"
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa kitengo cha (Shule Direct) na Former miss Tanzania, Faraja Nyalandu, alipokutana na wanamikakati wa kitengo cha Reach for change" nchini Sweden.
Semina hiyo iliyohudhuriwa na wanaharakati mbalimbali duniani, lililenga katika suala la kuinua Elimu kwa kila mtoto nchini Tanzania na Africa nzima kwa ujumla. Semina hiyo pia ilielezea mbinu na changamoto mbalimbali zinazo tumika ili kila mtoto aweze kupata elimu bora na si bora elimu.
Reach for Change" wakishirikiana na SIDA, waliandaa semina hiyo pia kupongeza nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kwa mafanikio na hatua kubwa waliopiga katika kugundua mbinu mbalimbali za kumuwezesha kila mtoto awe na uwezo wa kusoma,
Faraja ambae ni mkurugenzi wa Shule Direct" amepongezwa kwa juhudi zake za kugundua mbinu na nyenzo mbalimbali za kumrahisishia kila mtoto awe na uwezo wa kujisomea mwenyewe ndani na hata nje ya darasa,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment