Siagi ya Karanga ni moja ya vitu mhimu jikoni katika nyumba nyingi siku hizi, inapendwa na kila mtu watoto na watu wazima. Mimi napenda zaidi kuitumia kwenye mkate lakini pia unaweza kuongeza siagi ya karanga kwenye karibu kila mboga ya majani, samaki na kadharika.
Ukiacha radha yake nzuri na tamu, siagi ya karanga ni chakula chenye afya na nguvu nyingi na isiyo na takataka zozote zisizohitajika na mwili. Kama wewe ni mtu unayependa kutumia vyakula vyenye afya basi hii siyo ya kukosa nyumbani kwako!
1. Hukufanya usijisikie njaa kwa muda mrefu
Ni jambo la afya kutumia Siagi ya karanga hasa katika mlo wako wa asubuhi kwa sababu itakufanya ujisikie umeshiba kwa masaa mengi zaidi. Protini na faiba vilivyomo kwenye siagi ya karanga vinaweza kukupunguzia hamu ya kutaka kula vyakula vingine visivyo vya afya au vyakula feki kwa lugha nyepesi.
2. Bora kwa afya ya Moyo
Usawa wa mafuta yasababishayo kolesto ni mdogo sana ukilinganisha na usawa wa yale mafuta yasiyosababisha kolesto katika siagi ya karanga na hivyo kupunguza uwezekano wa mtu kupatwa na matatizo ya moyo. Vitamini E ipatikanayo katika siagi ya karanga ni mhimu sana katika afya ya mfumo wako wa upumuwaji.
3. Siagi ina Mafuta safi
Watu wengi huogopa kutumia siagi ya karanga sababu ya kuwa na kiasi kingi cha mafuta. Lakini ukweli ni kuwa mafuta yaliyomo kwenye siagi ya karanga ni mafuta safi ‘healthy fats’. Asilimia ya mafuta haya yasiyo na kolesto katika siagi ya karanga ni kubwa zaidi na hivyo unaweza kuitumia bila wasiwasi wowote.
4. Ina kiasi kingi cha faiba
Matumizi ya kiasi cha kutosha cha faiba ni mhimu kwa ajili ya ufanyaji kazi mzuri wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Siagi ya karanga ni chanzo kizuri kabisa cha faiba kwa ajili ya mwili.
5. Ina viinilishe vingi mhimu
Siagi ya karanga ina viinilishe vingi na ambavyo ni mhimu sana kwa mwili kama vile faiba, protini, potasiamu, kiuaji sumu, mafuta yenye afya, magnesium na vingine vingi. Viinilishe hivi ni mhimu kwa ajili ya utengenezaji na uimarishaji wa mifupa, kuimarisha mishipa na kuimarisha kinga ya mwili.
No comments:
Post a Comment