Inasemekana watu 11 wamefariki dunia papo hapo katika ajali iliyotokea mapema leo katika eneo la konakali, Mkanyageni Tanga. ajali hiyo ilihusisha gari ya abiria aina ya Costa, iliyogongana uso kwa uso na Scania Semitrera.
Kwa mujibu wa mashuhuda katika ajali hiyo, Costa imekatika kati kwa kati, na kwamba watu waliofariki ni wale waliokuwemo kwenye kosta hiyo.
Costa hiyo inayofanya safari zake Tanga mjini, kuelekea Lushoto.
Habari hizo zimeongeza kuwa hali ya majeruhi katika ajali hiyo ni mbaya
Imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi.
CRD . Kengete Blog
No comments:
Post a Comment