Friday, 17 October 2014

WATOTO MILIONI 21 KUPEWA CHANJO YA SURUA

Zaidi ya nusu ya wananchi kesho wanatarajiwa kuanza kupatiwa chanjo ya surua na rubella katika vituo vyote vya afya nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Donald Mbando alisema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inatarajia kuwafikia watoto zaidi ya milioni 21 wenye umri kuanzia miezi tisa hadi chini ya miaka 15 katika kampeni shirikishi ya surua na rubella itakayodumu kwa wiki moja.
Alisema sambamba na chanjo hizo, kutakuwa na utoaji wa matone ya vitamin A na dawa za kukinga magonjwa ya minyoo, matende na ngirimaji katika mikoa 16 yenye maambukizo makubwa ya magonjwa hayo na walengwa ni walio na umri wa miaka mitano na kuendelea.
“Ugonjwa wa surua bado ni tatizo kubwa nchini hasa kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano. Idadi ya watoto wasiokamilisha chanjo, imeendelea kuongezeka na kusababisha hatari ya kutokea kwa milipuko ya ugonjwa huo,” alisema. Dk Mbando. Aliongeza kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha magonjwa yanayodhibitika kwa chanjo, yanatokomezwa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!