Friday, 10 October 2014

VYAKULA VINAVYOFAA MGONJWA WA KISUKARI


Kisukari ni ugonjwa sugu ambao huathiri uwezo wa mwili kutumia nguvu na chakula kwa muda mrefu kutokana na kuongezeka kwa sukari aina ya glucose kwenye mishipa ya damu.




 Hii hutokana na mwili kushindwa kutengeneza hormoni ya insulini au kushindwa kutumia insulini iliyopo mwilini ambayo husaidia kupunguza sukari kwenye damu na kuwezesha matumizi yake. Kiasi kikubwa cha sukari kwenye damu huathiri mishipa midogo ya damu kwenye figo, miguu, moyo, macho na mfumo wa fahamu na hatimaye kusababisha kifo. 

Kumbuka kuna aina tatu za kisukari, 
1. Aina ya kwanza ni ile ya kuzaliwa nayo inayosababishwa na kinga ya mwili kuharibu uwezo wa kongosho kufanya kazi. 
2. Aina ya pili ni ile inayotokana na mfumo wa maisha asa uzito na unene kupita kiasi, au kula vyakula vyenye sukari mara kwa mara na kutofanya mazoezi inayosababisha vipokezi vya insulini kushindwa kufanya kazi.
3.Aina ya tatu ambayo sio kawaida ni pale sukari inapoongezeka kupita kiasi kwa mama mjamzito ambaye hakuwa na ugonjwa huu katika miezi mitatu ya mwanzo.
DALILI 
Unaweza kujitambua mapema kama unasumbuliwa na ugonjwa wa kisukali kwa kuwa na dalili zifuatazo:-
Kupungua uzito kwa kasi 
Kuisi njaa mara kwa mara
Kukojoa mara kwa mara.
Kuisi kiu na njaa mara kwa mara.
Kushindwa kuona vizuri au kuona mawenge.
Uchovu na maumivu ya kichwa.
MATIBABU.
Tiba ya ugonjwa huu inahusisha dawa zenye insulini na zile za kupunguza sukari kwenye mishipa ya damu, mazoezi, kurekebisha uzito, presha na lishe kwa ajili ya kupunguza madhara yatokanayo na ugonjwa huu.
LISHE INAYOMFAA MGONJWA WA KISUKARI.
Mgonjwa anatakiwa kupunguza kula vyakula vyenye protini na mafuta kwa wingi na kula vyakula vyenye nyuzinyuzi, nafaka, mboga za majani, matunda na vyakula vyenye mafuta kiasi ambavyo husaidia kuongeza damu na kupunguza sukari mwilini.
Epuka matumizi ya pombe, sigara, tumbaku na madawa ambayo hushusha kinga ya mwili kupigana na maambukizi.
Epuka vyakula vyenye sukari na usile chakula kingi. unaweza kula kidogo kidogo kulingana na matumizi ya dawa.
Punguza kiasi cha chumvi kwenye chakula na kununua vyakula vilivyotengenezwa tayari.
Maharage, samaki, mtindi, soya  nyanya, mayai na wali pia ni vyakula visivyo na ghalama sana na ni salama kwa mgonjwa wa kisukari.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!