Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas
Kiongozi wa matukio ya ulipuaji wa mabomu na umwagiaji tindikali viongozi wa dini aliyejulikana kwa jina la Yahaya Hassani Omary ameuwawa na jeshi la polisi wakati alivyokuwa akijaribu kukimbia.
Akithitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas Alisema kuwa tukio hilo limetokea October 19 majira ya saa tano na nusu katika barabara ya babati mkoani Arusha wakati alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo wa ugaidi alishikiliwa wiki mbili zilizopita huko mkoani Morogoro mara baada ya kutafutwa kwa muda mrefu na hapo jana alikuwa akipelekwa wilayani kondoa mkoani Dodoma kwa ajili ya kwenda kuonyesha sehemu ambazo alikuwa ameficha mabomu mengine.
"mtuhumiwa huyu alikuwa anasakwa kwa muda mrefu bila mafanikio kwani alikuwa akai sehemu moja ila jeshi la polisi huko mkoani morogoro lilimkamata wiki mbili zilizopita na baada ya kufanyia mahojiano alisema ameficha mabomu mengine huko kondoa na jana alikuwakipelekwa kuonyesha ndipo alipotumia trikizake ambazo amefundishwa za ugaidi kwa kupiga gudo na kutaka kuwakimbia askari ndio akapigwa risasi mbili"alisema Sabas
Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua waovu ili kuwaza kuteketeza matukio ya uhalifu
Chanzo: woindeshizza blog
No comments:
Post a Comment