Saturday, 18 October 2014

MTANZANIA ANAYEISHI NCHINI AUSTRALIA AUA WATOTO WAKE WAWILI KATIKA HALI YA KUSTAAJABISHA!


Raia wa Tanzania anayeishi katika jiji la Melbourne, Australia, Charles Amon Mihayo, 36, aliwanunulia binti zake Savannah, 4, na Indianna, 3, gauni za dance ya ballerina, akawaangalia wakidansi, kisha akawaua wote wawili kwa kuwakaba. 



Baada ya kuwaua mabinti hao, Mihayo aliwapigia simu polisi kuwataarifu, kisha aliiogesha miili ya marehemu, na wakati akiivalisha nguo miili hiyo, aliwaambia polisi waliofika na kugonga mlango, wasubiri kidogo.

 Alipofungua mlango, polisi walimuuliza, kwanini amewaua watoto wake. Mihayo alijibu kuwa hakuna “good reason for what he did but it made sense to him at the time” [hakuwa na sababu ya maana ya kuwaua, lakini aliona ni kitu cha busara wakati anafanya mauaji hayo.] 




Savannah,4, na Indianna, 3, enzi za uhai wao

Mtuhumiwa alisema kuwa hakupanga kuwaua binti zake, lakini hiyo haijalishi sasa maana maji yameshamwakiga; na kwamba hakutakiwa kufanya vitendo hivyo lakini ndio imeshatokea.

Dakika tisa baada ya Mihayo mwenyewe kuwapigia simu polisi na kuripoti kuwaua wanae, mama wa watoto hao aliwapigia simu ya dharura polisi kuwataarifu kuwa kuna kitu kimewatokea wanae waliokuwa wameenda kumtembelea baba yao.
 Ripoti ya polisi inasema siku moja kabla ya tukio, Mihayo alimtumia text-message mama wa wanae, ambaye ndiye aliyekuwa akiishi na watoto hao, kumuomba awapeleke watoto wakamtembelee ili awaone mara ya mwisho.

 Kabla ya kukutana, Mihayo aliwanunulia watoto hao gauni na viatu. Mama na watoto walipofika nyumbani kwa Mihayo, apartment ambayo amepangisha kutoka kwa bibi wa wanae, Mihayo alimuuliza mzazi mwenza ana muda kiasi gani na wanae, kisha akawaingiza ndani. 



Mama na bibi waliwasikia watoto wakicheza, kabla ya mmoja wa watoto hao kutoka barazani akiwa amevaa gauni ya maua na viatu vyeupe alivyonunuliwa na baba yao.

 Mtoto huyo alianza kudansi kabla ya baba yake kumuita arudi ndani, ili ajitayarishe kumuonyesha mama kitu kingine dakika kumi baadae.
 Baadae kidogo, mama na bibi waliona watoto wamekuwa kimya. Mama aligonga mlango, Mihayo akamwambia asubiri kidogo. Mama huyo akagonga tena. Mihayo akafoka “utajua watakapofika hapa!” Akimaanisha polisi. Mama alikimbilia kwenye sebule ya mama yake na kuwapigia simu polisi. Polisi, ambao tayari walishapigiwa simu na Mihayo mwenyewe, walipogonga mlango, Mihayo aliwajibu “I’m just finishing up.”




Marehemu Savannah na Indianna, wakiwa na mama yao

 Alipofungua mlango, huku akifuta mikono yake na taulo, aliwaambia polisi: “tayari nimemaliza…Nimeshawaua” [It's done, I've killed them.]
 Mihayo, ambaye alikiri kuwaua watoto hao kwa kuwakaba baadae aliwaambia polisi kuwa alikuwa amefurahia mama watoto kuwaleta wanae, ili aseme “goodbye” kwao kwa mara ya mwisho. Mihayo aliwaeleza kuwa aliwavalisha wanae gauni za ballerina na mabinti wakaanza kudansi. “Walienda nje kumuonyesha mama yao nguo zao mpya” alisema Mihayo. Alisema kuwa watoto waliporudi ndani, alirekodi video na simu yake watoto hao wakidansi nyimbo ya “Let it Go” kutoka kwenye movie “Frozen.”
 Mihayo alisema baada ya nyimbo kwisha, watoto hao walianza kucheza mchezo wa “hide and seek”(unafanana na kombolela.) Hapo ndipo alipoweka mto nyusoni mwa watoto wote wawili, na kuwabana mpaka walipoacha kuhangaika na kupumua.




Picha ya kuchorwa ya Charles Mihayo akiwa mahakamani. 

Camera haziruhusiwi mahakamani
 Baada ya watoto hao kupoteza maisha, Mihayo aliwapigia simu polisi, na kuwapeleka watoto hao bafuni na kuanza kuwaogesha na kuwavalisha nguo.
 Mihayo hakutoa sababu za mauaji hayo zaidi ya kusema wapelelezi hawawezi kuelewa “what he has been through” na kwamba kutoa sababu ya mauaji haitabadilisha chochote.


 Mihayo anashikiliwa mahabusu, akisubili kutokea mahakama kuu kukabiliana na tuhuma siku za usoni.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!