Friday, 31 October 2014

NSSF KUJENGA KIJIJI CHA BUNGE



SHIRIKA la Hifadhi ya Jamii (NSSF) inakamilisha mchakato wa kuanza ujenzi wa kijiji cha Bunge mjini Dodoma na upanuzi wa ofisi ndogo ya Bunge Dar es Salaam.



Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa NSSF kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2012/13 na hesabu zilizokaguliwa, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dk Ramadhan Dau alisema kinachosubiriwa ni uteuzi wa makandarasi utakaofanyika mwanzoni mwa mwaka 2015.
“Michoro na nyaraka za zabuni zimekamilika kwa ujenzi wa kijiji cha Bunge, hatua inayofuata ni kuitisha wazabuni ili kupata makandarasi wa ujenzi. Na kwa upanuzi wa ofisi kazi ya kuandaa michoro itakamilika Aprili 2015,” alisema.
Dau alisema shirika lake pia litajenga ofisi za wabunge majimboni ambapo michoro na nyaraka za zabuni zimekamilika na kinachosubiriwa ni uteuzi wa makandarasi.
Aidha, Dau alisema NSSF pia inasubiri kupewa kibali cha ujenzi wa jengo la ubalozi Nairobi lenye majengo mawili yenye ghorofa 22 na 12.
“Pia Shirika linasubiri majibu ya Serikali kupitia Stamico kutokana na maombi ya kuwa mbia katika uwekezaji kwenye mgodi wa Kiwira baada ya Stamico kutangaza kutafuta mbia,” alisema.
Akizungumzia changamoto, Dau alisema NSSF inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwepo ongezeko la mafao ya kuacha uanachama jambo ambalo linasababisha wastaafu kukosa sifa ya kupata pensheni na kuwa tatizo hilo linaweza kuleta athari ya maendeleo ya nchi kwa kuwa na idadi kubwa ya wazee ambao hawana kipato chochote.
Aidha, Dau alisema katika mwaka wa fedha 2012/13, NSSF ilikusanya Sh milioni 476,107 ikiwa ni ongezeko la asilimia 13.29 ukilinganisha na mwaka 2011/12 katika mapato yatokanayo na michango ya wanachama.
NSSF imelipa mafao kwa wanachama wake yanayofikia Sh milioni 228,049 ikiwa ni ongezeko la 27.62 ukilinganisha na mafao ya Sh milioni 178,692 yaliyolipwa mwaka wa fedha 2011/12. Kuhusu ukuaji wa mfuko, Dau alisema:
“Thamani ya Mfuko umeongezeka kutoka Sh milioni 2,108,801 mwaka 2011/12 na kufikia Sh milioni 2,470,149 2012/ 13 ikiwa ni ongezeko la asilimia 17.13.

CHANZO: HABARI LEO

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!