Wednesday, 22 October 2014

MTUHUMIWA WA MAUAJI AOMBA KUJUA HATIMA YAO

 
Mshtakiwa wa mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi, Longishu Losingo ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ieleze lilipo jalada la kesi yao na hatima yake ni nini.
Longishu aliyaeleza hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema muda mfupi baada ya wakili wa Serikali, Leonard Challo kuieleza Mahakama kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Alidai kuwa mwaka mmoja umepita, hawajui jalada la kesi yao liko wapi na limefikia katika hatua gani.
“Sisi tunateseka huko gerezani, tunateseka hakuna starehe gerezani,” alisema Longishu.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Lema aliiahirisha kesi hadi Novemba 5 mwaka huu, itakapotajwa tena kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika au la.
Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Masunga Makenza (40), Chibago Magozi (32), John Mayunga (56) Juma Kangungu (29), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40), Zacharia  Msese (33), Msungwa Matonya (30) na Ahmad Kitabu (30).
Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa Novemba 3, mwaka jana walifanya kosa hilo la mauaji kinyume na kifungu cha 196 cha sheria na kanuni ya adhabu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!