Mungu anaposema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hamaanishi maarifa ya kutengeneza au kuendesha ndege, ni maarifa ya kawaida tu katika maisha yetu ya kila siku ambayo yanaweza kubadilisha afya na ustawi wetu. Moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na viinilishe vingi na mhimu sana kwa afya ya binadamu ni kitunguu swaumu. Kitunguu swaumu ni dawa karibu kwa kila ugonjwa.
Huko sokoni tayari nimeviona vitunguu swaumu kutoka China na Afrika kusini ambavyo vyenyewe huwa vina punje kubwa nene na huwa rahisi kuvimenya, hata hivyo ili upate faida hizi zote hapa chini naendelea kukushauri utumie vitunguu swaumu vyetu vinavyolimwa hapa Tanzania kwani hivyo vya kutoka nje pamoja na kuwa ni rahisi kuvimenya lakini ubora wake si kama ule wa vitunguu vyetu.
Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuipuwa mboga yako toka katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake. Kama una friza au friji ya kawaida unaweza kumenya vitunguu swaumu hata kilo nzima na kuvitwanga kidogo katika kinu, vifunge vizuri katika bakuli au mfuko wa plastiki na uvihifadhi katika friza au friji na hivyo kila unapopika unachukuwa tu na kukitumia ili kuepuka usumbufu wa kukimenya kila siku.
Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji kikiwa kibichi. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja na ukigawe mara 2, menya nusu yake (punje 15 mpaka 20), menya punje moja baada ya nyingine na kisha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu kisha meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala au fanya kutwa mara 2 kama unaumwa na moja wapo ya magonjwa niliyoyaorodhesha hapa chini. Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo utakuwa mbali na kuuguwauguwa.
Haya ni baadhi ya magonjwa yanayotibika au kukingika na kitunguu swaumu:
- Huondoa sumu mwilini
- Husafisha tumbo
- Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
- Husafisha njia ya mkojo
- Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria
- Huzuia kuhara damu (Dysentery)
- Huondoa Gesi tumboni
- Hutibu msokoto wa tumbo
- Hutibu Typhoid
- Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
- Hutibu mafua na malaria
- Hutibu kifua kikuu
- Hutibu kipindupindu
- Hutibu upele
- Huvunjavunja mawe katika figo
- Hutibu mba kichwani
- Huupa nguvu ubongo
- Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
- Huongeza SANA nguvu za kiume
- Hutibu maumivu ya kichwa
- Hutibu kizunguzungu
- Hutibu shinikizo la damu
- Huzuia saratani/kansa
- Hutibu maumivu ya jongo/gout
- Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
- Huongeza hamu ya kula
- Huzuia damu kuganda
- Husaidia kutibu kisukari
- Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi
- Huongeza SANA kinga ya mwili
No comments:
Post a Comment