Shughuli ya upatikanaji wa vitambulisho vya uraia nchini Tanzania imegeuka kuwa kero kwa wananchi badala ya faraja waliyoisubiri kwa hamu.
Kumekuwa na msongamano wa watu katika maeneo mbali mbali wanaoitwa kupokea vitambulisho vyao bila mafanikio.
Kwa Zaidi ya miaka miwili sasa tangu vitambulisho hivyo vianze kuandaliwa na hatimaye kutolewa, kumekuwa na changamoto upande wa uhakiki taarifa na uhaba wa vifaa walivyopewa NIDA na serikali ya Tanzania kama vitendea kazi.
Vifaa vilivyotarajiwa kwa zoezi zima la usajili na utoaji wa vitambulisho nchini Tanzania ni elfu tano lakini kwa sasa vilivyopo ni miatano tu kwa nchi nzima yenye mikoa Zaidi ya 26.
Msongamano wa raia wa Tanzania mbele ya kituo cha kupokea kadi za utambulisho wa raia,bila kujali mwanamke ama mwanaume mzee au kijana ,mjamzito ama mzazi wote mchapalo pasi na tafrija, macho mlangoni kusubiria nani atatoka wa kwanza kwenye kadhia ya kukaribiana kwa saa moja hadi saa mbili,mradi kitambulisho kitoke na maisha yaendelee.
Mayasa Kimbau yeye ni mjasiriamali ambaye amelazimika kufunga biashara yake kwa muda wa siku mbili bila shurti ili akomae kwenye msongamano Na kufuatilia kitambulisho chake na huku akiwa na motto wake mdogo ambaye ni mgonjwa aliye ambatana naye katika msongamano huo wa kusubiria kitambulisho chake.
Shaaban Chike ni mkaazi wa jiji la Dar-Es-Salaam kwa muda wa miaka 26 sasa, amefuatilia kitambulisho hicho kwa siku mbili mfululizo bila mafanikio na kuuita utaratibu wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa la Tanzania kuwa ni wa ajabu na ambao hajawahi kuuona kwa kipindi chote cha uhai wake.
Naye mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa la Tanzania NIDA,Dickson Maimu anasema shughuli nzima ina mafanikio katika usajili na hatimaye utoaji wa vitambulisho.
Hata hivyo shughuli hiyo imejaa changamoto, moja wapo ikiwa ni vifaa vya kuchukulia alama za kibaiolojia kuwa ni vichache ,usajili mgumu ikiwemo makaratasi yenye majina kuchanwa usiku wa manane na hivyo kuleta usumbufu kwa wananchi na mamlaka yake, na pia uwekaji wa kumbukumbu kwenye mfumo wa mamlaka hayo ni shida .
Vitendea kazi vya mamlaka hayo ni mia tano tu wakati vinavyohitajika ni elfu tano,viliweza kuzunguka Zanzibar,Dar-Es-Salaam na sasa ni mkoa wa pwani na ili kupunguza kadhia ya usajili wa kibailojia serikali ya Tanzania imeahidi kuongeza vitendea kazi elfu mbili na miatano na hivyo kufanya idadi ya vitendea kazi hivyo kufikia elfu mbili na miatano na kufikisha nusu ya idadi husika.
No comments:
Post a Comment