.jpg)
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema matokeo ya sensa ya watu na makazi yanaonyesha kuwa idadi ya wanawake inaendelea kuongezeka kulinganisha na wanaume.
Hayo yalibainishwa mjini hapa jana na mkurugenzi mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa.
Idadi ya wanawake Tanzania Bara ni 23,058,933 na wanaume 21,869,990.
Alisema Tanzania ina watu 44.9 milioni, Tanzania Bara ikiwa na watu milioni 43.9 na Zanzibar milioni 1.3.
Alisema mkoa unaoongoza kwa kuwa na watu wengi ni Dar es Salaam ukiwa na watu milioni 4.3 pia ukifuatiwa na Mwanza wenye watu milioni 2.7.
Alisema watakuwa wakipita mkoa kwa mkoa kutoa matokeo hayo ya sensa kwa lengo la kumfikia kila mdau ili aweze kuzitumia takwimu kwa kupanga mipango yake binafsi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza aliwataka wakuu wa wilaya na viongozi wote wa halmashauri na vijiji kuhakikisha wanatumia vizuri takwimu za sensa kwa ajili ya maendeleo ya mkoa.
MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment