Utafiti uliofanywa umeonyesha kuwa kula ndizi mbili zilizoiva kwa siku utaweza kufanya kazi za nguvu kwa dakika 90 mfululizo au kuwawezesha wanariadha kukimbia mbio fupi na ndefu.
Vilevile ndizi mbivu zina virutubisho vya kusaidia kupambana na maradhi kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na Wamarekani na kuwekwa kwenye tovuti ya habari za afya ya www.medical.news.
“Hii ni kwa sababu ndizi zina aina ya protini inayojulikana kama tryptophan. Tryptophan hubadilishwa kuwa seroton, inayomfanya mtu ajisikie mwenye raha kwa kujipumzisha na kuwa na faraja,” inaeleza sehemu ya utafiti huo.
Kwa hiyo, wanashauri watu kuachana na kumeza vidonge hasa unapojisikia mchovu na kula ndizi ili uwe na faraja.
Ndizi husaidia kutuliza mfadhaiko wa mawazo, huufanya mwili kuwa na nguvu na kurekebisha kiasi cha sukari kwenye damu, huzuia mkakamao wa misuli wakati wa kazi, huongeza kalisi inayopotea wakati wa kukojoa na huimarisha mifupa.
Ndizi husaidia kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu, hupunguza ugonjwa wa upungufu wa damu kwa kuongeza madini ya chuma, hupunguza shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo na husaidia kumeng’enya vyakula.
Hupunguza maumivu yatokanayo na vidonda vya tumbo husaidia kuzuia saratani ya figo na kulinda uharibifu wa misuli ya macho.
Humuwezesha mwanafunzi kuwa makini kwa kuwa ndizi zina kiwango kikubwa cha kalisi, vitamin na magnesi. Ndizi huweza pia kutumika kung’arisha viatu na mabegi kwa kutumia upande wa ndani wa ganda la ndizi na baadaye tumia kitambaa kikavu kwa ajili ya kung’arisha.
Imeandaliwa na Stephen Maina
CRD. MWANANCHI
No comments:
Post a Comment