Je wewe ni miongoni mwa wapenzi wa choroko? Kama unatumia utakuwa miongoni mwa wanaofaidika na virutubisho muhimu kwa afya mwilini.
Wataalamu waliofanya uchunguzi kuhusu choroko ambayo ni jamii ya kunde,
wanasema utamu wa ladha yake unashabihiana kabisa na umuhimu wake katika afya.
Choroko ni kati ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha protini, madini ya phosphorus na calcium. Ukiachilia mbali faida nyingine, virutubisho hivi ni muhimu sana kwa ustawi wa afya ya ubongo.
Wataalam mbalimbali wamenukuliwa na mtandao wa kesehatan.123.com wakielezea umuhimu wa ulaji wa choroko ili kuongeza uwezo wa kufikiri.
Faida nyingine za choroko ni pamoja na kuimarisha mifupa. Hii inatokana na kiwango kikubwa cha madini ya phosphorus na calcium.
Choroko pia ni nzuri kwa afya ya moyo, mafuta yaliyopo kwenye mboga hii ni salama na yana faida katika kuusaidiana moyo kutenda kazi zake vizuri na kwa upande mwingine kusaidia kurahisisha ufyonzwaji wa chakula mwilini hivyo kuepuka hatari ya kupata saratani.
Uwepo wa vitamin B1 na B2 ndani yake husaidia kuimarisha mfumo wa fahamu nasi vizuri kutumiwa na wajawazito kwa sababu zina kiwango kikubwa cha folic acid ambayo ni muhimu kw aukuaji wa mtoto.
Mapishi ya choroko
Mahitaji
Choroko kikombe 1 na nusu
Nazi kopo 1
Kitunguu kikubwa 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum 1 kijiko cha chai
Curry powder 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Olive oil
Pilipili nzima
Matayarisho
Loweka choroko usiku mzima kisha zichemshe mpaka ziive na ziweke pembeni. Baada ya hapo saga pamoja nyanya, kitunguu, na swaum kisha vipike mpaka maji yote, baada ya hapo tia mafuta na curry powder, pika mpaka nyanya zitoe mafuta kisha tia choroko,tui la nazi, maji nusu kikombe,pilipili na chumvi, kisha koroga vizuri na uache ichemke. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na rojo ibakie kidogo sana, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Mi huwa napenda kuila na wali ila hata na ugali au chapati inaenda pia.
No comments:
Post a Comment