Sunday, 28 September 2014

WAZO LA LEO! SIRI YA MAFANIKIO


1. ACHA KUWA NA MARAFIKI
WANAOKUPOTEZEA MUDA
Watu wengi tumekuwa na marafiki wengi
sana na marafiki ni mhimu sana katika
maisha yetu haya wapo wanaotufaa na
wasiotufaa kuwa na marafiki wanao
weza kukusaidia na kukupa hamasa ya
kimaendeleo ,malengo yako na kuwa na
maisha Fulani. Hivyo achana na marafiki
wasio kuwa na msaada kwako.


2. ACHA KUKIMBIA MATATIZO YAKO
Waswahili wanasema kuwa “kukimbia
tatizo si kutatua tatizo” Hivyo basi kama
tatizo umekutana nalo basi tafuta njia ya
kulitatua tatizo hilo kwani matatizo
hayaji kuisha katika dunia hii kama
unakimbia utakimbia mangapi ?
Unatatizo la pesa kwanini usitafute pesa
ila kama hufanyi kazi unategemea kupata
pesa huwezi. Matatizo hayaepukiki
komaa na ulitatue utajikuta kama uko
peke yako katika hii dunia lakini kuna
watu wana matatizo zaidi yako na
wanahangaika kuyatatua.

3. ACHA KUJIDANGANYA MWENYEWE
Katika maisha ya sasahivi unaweza
kumdanganya mtu yeyote yule lakini ogopa
sana kujidanganya. Vijana wengi
tumekuwa tukijivuna mbele za watu kuwa
tuna hili mara lile ili mradi tu tuonekane
ni watu wazuri kwa watu wanao
tusikiliza.

4. ACHA KUIGA MAISHA YA WATU
WENGINE
Vijana wengi hili kwetu limekuwa janga
kubwa sana maisha yetu yamekuwa
yakuigiza sana (copy and paste) hasa
hasa tunapenda kuonekana ni watu
Fulani wenye maisha mazuri, hatuzijui
shida ni watu wakula bata wakati si
kweli. Maisha yetu yamekuwa magumu
na yatakuwa magumu kwasababu ya
kuiga maisha ya watu wengine ishi
maisha halisi uliyonayo watu wakajua
asili yako siyo kuigiza unaweza kosa
kusaidiwa na watu.

5. ACHA KUKUMBUKA YALIYOPITA
Hapa kuna mambo mengi tunajifunza
wengi hukumbuka yaliyopita hasa waliyo
shindwa kuyafanya au yaliyowaumiza
kwa kukumbuka yaliyopita haiwezi
kukusaidia kwani kila tuamkapo asubuhi
ni kama tumezaliwa upya na siku ni
nyingine,tarehe na mambo
utakayoyafanya ni mengine si sawa na
jana. Waswahili wanasema “Tusahau
yaliyopita tugange yajayo” hii ina maana
kuwa wewe si wa kipindi kile bali ni
mwingine na akili ni mpya.

6. ACHA KUOGOPA KUFANYA MAKOSA
Makosa ndiyo walimu wetu mkubwa
sana katika maisha yetu na kila
binadamu si mkamilifu toka uzaliwe
mpaka sasa kuna makosa mengi
uliyoyafanya na kupitia makosa hayo
umejifunza kutorudia makosa tena na
makosa hutujenga zaidi na kuwa makini
zaidi kama ukifanya kosa huna haja ya
kujilaumu chukua muda kujilekebisha na
kusonga mbele kosa lisiwe tatizo la
kukukatisha tamaa.

7. ACHA KUNUNUA FURAHA
Vitu vingi tunavyo vihitaji vinagharama
kubwa sana na vitu hivyo si kwamba
tuna vipenda bali ni tamaa tu tuliyonayo
na hiyo yote ni kuamini kuwa furaha ya
maisha tutaipata huko si kweli. Mungu
alitupatia furaha, na upendo bure ni vitu
unavyozaliwa navyo fikiria kama
vingekuwa vinauzwa wangapi? Wangapi
tungekuwa hatuna furaha. Hivyo basi
anza kuyafurahia maisha yako hivyo
vingine vitakufuata.

8. ACHA KUSHINDANA NA MTU
KIMAISHA
Acha kushindana na mtu kimaisha
haitakusaidia huwezi jua yeye anafanya
nini kuzipata pesa zake au mali zake na
wewe unazipataje ushindani mzuri katika
maisha ni ule wa kwako na mafanikio
yako jiangalie kile unachokifanya na
matokeo yake unapata nini? huo ndio
ushindani mzuri kuliko wote sio
kushindana na mtu kimaisha acha.

9. ACHA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO
YASIYO SAHIHI
Katika mahusiano si kitu cha kujiingiza tu
au kama unaoa si kuoa tu kwasabu
Fulani kaoa basi na mimi nioe, si kudai
kuwa nimechoka kufua ngoja nioe sasa
ndiyo maana karne hii inaongoza kwa
wanandoa kuachana na ndoa za utotoni
kwasababu watu hawajipangi ni kuiga tu.
Mahusiano au ndoa ni kitu kikubwa sana
na kama umempenda mtu onyesha kuwa
unampenda kweli mtangulize mbele yako
kuwa ndiyo kila kitu kwako/ kila kitu
kinaenda kwa ajiri yake. Kama unaingia
katika mahusiano mheshimu mwenzako
na kumpenda mpe nafasi kubwa katika
maisha yako.

10. ACHA KUJILAUMU
Kuacha kujilaumu ni njia mojawapo ya
kufanikiwa katiaka maisha yako unapo
kosea amini kuwa wewe si mkamilifu na
hakuna binadamu aliyekamilika jipange
songa mbele. Wagunduzi wa vifaa
mbalimbali vinavyotumika kama vya
umeme na vinginevyo si kwamba hawa
kufanya makosa walikosea sana mpaka
kutoa kitu sahihi .

11. ACHA KUONGELEA YA WATU FULANI.

Kuzungumzia maisha ya mtu Fulani
haikusaidii ni kupoteza muda tu kwanini
usiwaze maisha yako unatakiwa kufika
wapi na ufanye nini kuishi maisha
mazuri unakaa na kuanza kuzungumzia
mtu Fulani yupo hivi mara hivi wakati
huo huyo mtu unaemsema yeye yupo
kazini we upo kijiweni mtalingana kweli?
Acha kuzungumzia maisha ya watu fanya yako ufurahie maisha.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!