Wahamiaji wengi kutoka Libya wameripotiwa kupoteza maisha yao baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kuzama ikielekea upande wa Italia.
Kwa mujibu wa wanajeshi wa majini wa Libya, watu hao walikuwa wakijaribu kuvuka kuelekea Ulaya.
Msemaji wa majeshi ya majini ya Libya, Ayub Qassem amethibitisha watu 36 wameokolewa baada ya mashua yao iliyokuwa imebeba watu 250 ilipozama karibu na eneo la Tajoura, mashariki mwa Tripoli.
Mkasa huu umetokea wiki chache tu baada ya mashua nyingine tatu kuzama mfululizo katika njia ya baharini inayotoka Libya hadi Italia.Hata hivyo, amefichua ya kwamba maiti nyingi bado zinaelea baharini.
Kumekuwa na ongezeko la watu wanaoikimbia nchi ya Libya mwaka huu kutoka na ghasia zinazoshuhudiwa, huku walunguzi wa binadamu wakipata fursa ya kutekeleza uhalifu wao.
Waasi wamekuwa wakipigania udhibiti wa miji na vituo muhimu nchini Libya.
Wamedai imewabidi kuazima mashua kutoka kwa wavuvi na kampuni nyingine.Wanajeshi wa majini wa Libya wamelalamikia ukosefu wa vifaa na uwezo wa kutosha wa kukabiliana na mikasa.
Bw. Qassem amefafanua ya kwamba wengi wa wahamiaji hao walikuwa waafrika na pia jinsia ya kike.
1 comment:
aziz bilal02:03
1
Reply
Wamkumbuke marehemu Moammar Ghadaff enzi zake mambo ka hayo yalikuwa hayatokei kabisa,Libya kwisha
Post a Comment