Monday, 15 September 2014

WAJAWAZITO WAJIFUNGUA KWENYE TENGA MKULANGA

WAJAWAZITO katika Kijiji cha Chamgoi, Kata ya Mkamba, wilayani Mkuranga, Pwani, wamekuwa wakijifungua njiani kwenye matenga kutokana na kukosa kituo cha afya.

Hayo yalibainika juzi kijijini hapo, baada ya Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kufanya ziara katika Kata hiyo kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama hicho.
Akizungumza na Tanzania Daima juzi kijijini hapo, Amina Abdalla, alisema hali hiyo inasababisha watoto wanaozaliwa kupoteza maisha kutokana na kukosa huduma ya kwanza pindi wanapozaliwa.
“Tunapotaka kujifungua tunaenda umbali wa saa tatu kufuata huduma hiyo, katika vituo vya jirani, usafiri hakuna hali inayotulazimu tupakiwe kwenye baiskeli au pikipiki ambapo tunawekwa kwenye tenga,”alisema.
Diwani wa kata hiyo, Hassan Dunda, alisema mpaka sasa wananchi wamejichangisha sh milioni 17 kwa ajili ya ujenzi wa zahati katika kijiji hicho na kwamba kwa sasa imefikia hatua ya kuweka milango na madirisha.
“Chamgoi hatujaridhishwa na serikali kutowaunga mkono wananchi, natoa wito kwa wanakijiji, msikimbilie kuchagua viongozi ambao wanaomba uongozi bila kujipima uwezo wao wa kuwatumikia alisema Dunda
ambaye pia ni Katibu Mwenezi wilayani humo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!