WATU wenye ulemavu wa ngozi (albino), wamekuwa wakisumbuliwa na maradhi ya ngozi hususan saratani ya ngozi.
Maradhi hayo hadi sasa, baadhi ya watu huyachukulia kuwa labda hayana tiba, hiyo inatokana na jamii kuwatelekeza wapatwapo na maradhi hayo.
Jamii inapaswa kutambua kuwa maradhi hayo yana tiba kinyume inavyodhaniwa na baadhi ya watu.
Kutokana na mazingira hayo, serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeweka mazingira mazuri ya kuwapatia matibabu watu hao wenye wenye ulemavu wa ngozi.
Mazingira hayo yatawasaidia albino kujikinga na ugonjwa huo wa saratani ya ngozi, kulinda afya zao.
Rai kama hiyo imekuwa ikitolewa mara kadhaa na baadhi ya wataalamu wa magonjwa hao. Miongoni mwa wataalamu hao baadhi yao ni madaktari Bingwa wa magonjwa ya ngozi na afya ya jamii kutoka Hosipitali ya Rufaa ya KCMC.
Kauli kama hiyo waliwahi kuitoa wakati akitoa huduma kwa walemavu wa ngozi katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure kupitia ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Standing Voice.
Ushari huo unapaswa kufanyiwa kazi kwa sababu idadi ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini ni kubwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Ieleweke kuwa maradhi ya saratani ya ngozi ni tatizo kwa taifa hata hivyo, waathirika wakitibiwa mapema wanaweza kuepuka kupata kansa hiyo.
Aidha, ni wakati kwa wadau na taasisi mbalimbali kuungana kuwasaidia kimatibabu albino ambao wanaonekana kupatwa na maradhi hayo.
Kwa mfano kulikuwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali lenye makao yake makuu nchini Uingereza (Standing Voice ni), limewahi kufadhili huduma hiyo.
Kipindi hicho shirika hilo liliamua kuwafadhili albino waliokuwa wakishindwa kusafiri kufuata huduma hiyo katika Hospitali ya KCMC au Ocean Road.
Tukubali kuwa tatizo hilo bado lipo na linazidi kukuwa katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo basi kila Mtanzania atumie nafasi yake kuwasaidia watu hao wenye ulemavu wa ngozi
TZ DAIMA
No comments:
Post a Comment