Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo wa mpira wa vikapu imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia yanayofanyika huko Korea Kusini baada ya kuagizwa kuvua hijab kabla ya mechi yao dhidi ya timu ya Mongolia .
Wanawake hao walikataa kata kata kuvua vazi hilo na wakajiondoa mashindanoni wakidai inakiuka maagizo ya dina ya Kiislamu inayomtaka mwanamke kujistiri nywele zake haswa akiwa faraghani.
Sheria za shirika la mchezo huo duniani haziruhusu kuvaliwaj kwa vitambaa vya kichwani wakati wa mechi lakini sasa wamekuwa wakijadili iwapo sheria hiyo itaondolewe.
Hata hivyo ilipowadia wakati wa mechi yao dhidi ya Nepal sheria hiyo haikuwa imebadilishwa na hivyo iliwabidi kuyaaga mashindano.
Fani nyengine za michezo katika mashindano hayo ya Bara Asia zinaruhusu uvaliwaji wa hijab.
Timu ya taifa ya unyanyuaji uzani ya Iran imekuwa ikishiriki mashindano hayo huku wakiwa wamevalia hijab.
Baraza la mashindano ya Olimpiki ya Bara asia OCA imesema kuwa haki za wachezaji ni zinapaswa kupewa kipaombele .
Baada ya kuyaaga mashindano hayo mchezaji wa Qatar Amal Mohamed A Mohamed alisema kuwa walikuwa wamehakikishiwa kuwa wataruhusiwa kushiriki mashindano hayo wakiwa wamevalia hijab na hivyo hawaelewi kwanini sheria hiyo haijabadailishwa.
''nina hakika kuwa hatutashiriki mashindano yeyote ya Bara Asia hadi sheria hiyo ibadilishwe''
Mashindano hayo hufanyika kila baada ya miaka 4 na huwaleta pamoja washiriki 9000 kutoka mataifa 45 yakishindana katika fani 36 ya michezo.
Mashindano hayo yatamalizika tarehe 4 Oktoba.
No comments:
Post a Comment