DA! Duniani kuna mambo jamani! Katika hali isiyo ya kawaida, maeneo ya Tandale Kwatumbo jijini Dar, waombolezaji hawakuamini macho yao wakati walipomuona ‘marehemu’ Mohamed Salum ‘Fido’ (29) (pichani), akirejea nyumbani hapo huku maandalizi ya mazishi yake yakipamba moto na waombolezaji, hasa mkewe, mtoto na ndugu wakilia kwa uchungu kufuatia ‘kifo’ chake.
Kijana Mohamed Salum ‘Fido’ anayesadikiwa kuwa alikufa.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, mwaka huu, saa sita mchana wakati shughuli mbalimbali za mazishi yake zikiendelea zikiwa ni pamoja na maandalizi ya chakula cha mchana kwa waombolezaji.
Iko hivi; Fido ni dereva wa bodaboda, kijiwe chake kikiwa Lumumba Mnazi Mmoja, Dar. Inadaiwa kwamba Septemba 10, mwaka huu alikamatwa na polisi wa ‘Tigo’, Lumumba kwa madai ya kutokuwa na kibali cha kuingia mjini, akapelekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central).
Pale kituoni, habari zinadai maafande hawakumruhusu kumpigia simu mkewe ili kumweleza yaliyompata, ndipo ndugu walipoamua kumtafuta kwa siku mbili bila mafanikio.
Septemba 11, mwaka huu, mkewe, kaka yake na baba yake mzazi walikwenda Hospitali ya Mwananyamala na kuingizwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) ambapo walioneshwa maiti moja! Vilio vikaibuka kwani wote walisema ni Fido. Marehemu huyo aliuawa kwa kugogwa na kitu kizito kichwani na maiti yake ilipelekwa hapo na polisi.
Ndugu hao walitoka na vilio hadi nyumbani na msiba ukawekwa kwa kukusanya mikeka na chakula kuanza kupikwa huku sehemu ya kuzikia makaburini ikitafutwa achilia mbali sanda kupatikana huku ndugu walio mbali wakijulishwa kuhusu msiba huo.
Siku ya tukio, watu wakiwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuufuata mwili, ndipo Fido alipoibuka na kusababisha tafrani kubwa.Baadhi ya watu waliingia mitini kwa woga huku ndugu wakishangaa iweje maiti itoke mochwari yenyewe? Ndipo Fido alipotangaza kwa sauti kuwa, hakufa, alikuwa polisi.
Akizungumza na Uwazi huku akifakamia msosi kwa madai kuwa hakula tangu alipokamatwa, Fido alisema alikamatwa na polisi lakini akakosa njia ya kuwasiliana na familia yake.
Naye mke wa marehemu alipopewa nafasi ya kusema alikuwa na haya:
Naye mke wa marehemu alipopewa nafasi ya kusema alikuwa na haya:
“Nimepigwa butwaa, siamini kama ndiye huyu mume wangu, watu wamekusanyika kwa ajili ya maombolezo, nilijua hatukonaye tena. Ama kweli Mungu mkubwa, nimefurahi kufika kwake nyumbani.
“Ilikuwa Jumatano saa 1.45 asubuhi mume wangu aliniaga na kwenda kazini kwake lakini hadi saa mbili usiku alikuwa hajarudi na si kawaida yake, ilikuwa nikipiga simu yake inaita tu.
“Ilikuwa Jumatano saa 1.45 asubuhi mume wangu aliniaga na kwenda kazini kwake lakini hadi saa mbili usiku alikuwa hajarudi na si kawaida yake, ilikuwa nikipiga simu yake inaita tu.
“Ilibidi niende Tandale wanakohifadhia pikipiki, nilikuta wenzake wamesharudisha pikipiki lakini yeye alikuwa bado.“Tulifuatana na ndugu zangu hadi Lumumba hatukumuona, tulienda Kituo cha Polisi Msimbazi, Central, Oysterbay na Kawe lakini walituambia hakuna mtu mwenye jina hilo aliyekamatwa ama kupatwa na tatizo, ilibidi twende Hospitali ya Mwananyamala mochwari kuulizia kama kuna maiti iliyookotwa.
“Uongozi wa mochwari ulitueleza kuna maiti tatu zilizopelekwa na polisi lakini hazifahamiki, moja ni kwa ajali ya pikipiki, mwizi kuuawa na wananchi na nyingine kuokotwa ufukweni mwa bahari ikiwa imefungwa kamba mikononi na kukatwa panga kisogoni.
“Mimi, baba pamoja na shemeji yangu tuliingia mochwari kuthibitisha. Tulipofika katika maiti iliyofungwa kamba na kukatwa panga kisogoni wote tulijiridhisha kuwa ndiye yeye kutokana na alama alizokuwa nazo, sikujua kilichoendelea, naamini nilipoteza fahamu baada ya kuuona mwili huo.
“Tulirudi nyumbani kuandaa msiba, kuweka maturubai, kununua sanda na kuandaa jeneza, tulipiga simu sehemu mbalimbali hadi mikoani kuwajulisha ndugu.“Tulijiandaa ili ndugu wa Morogoro na mikoa mingine wakija katika mazishi yaliyotarajiwa kufanyika kesho Ijumaa (iliyopita) katika makaburi ya hapa Tandale ambapo tulishapewa eneo la kuchimba kaburi.
“Kweli sijui nisemeje, tuliwataka radhi waombolezaji kwa usumbufu, baadhi walitawanyika kwa wakati huo wengine waliendelea kuwepo hata ndugu zetu wengine wako njiani wakitokea Mbeya na Mtwara.”
1 comment:
aziz bilal21:59
1
Reply
Jeshi letu la police lielimishwe kuhusu umuhimu wa simu na kutoa habari sio kukamata watu na kuwazuia kuwasiliana na ndugu zao au jamaa
Post a Comment