Wake wa Marais pamoja na viongozi wametakiwa kuchukua hatua, kutumia sauti zao na nafasi yao ili kuhakikisha watoto, wasichana na wanawake wanapata elimu na afya bora na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
Mwito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwenye mkutano uliojadili jinsi gani Dunia ichukue hatua kwa ajili ya afya na uchumi wa wanawake na wasichana uliyofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Jengo la Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York.
No comments:
Post a Comment