Friday, 26 September 2014

CHAKULA BORA KWA MTOTO WA MWAKA MMOJA NA ZAIDI

014









Uji ni wa kawaida kabisa kwa watanzania wengi,Mara nyingi hutumika kama kifungua kinywa au mlo  mdogo wa saa kumi jioni.Uji kwa upande mwingine ni chakula kikubwa kwa watoto wachanga,mara nyingi uji huwa chakula cha kwanza mtoto kujifunza kunywa  baada  ya maziwa,pia hutumiwa sana na wajawazito na wagonjwa.Uji pia ni chakula kikubwa sana kwa baadhi ya makabila,wajaluo wenzangu naamini mtaniunga mkono nikisema bila uji maisha hayasongi.

Unga ndio kiungo kikuu cha uji ,haijalishi unga huo umetokana na nini,unaweza kua  wa mchele,mahindi,maharage,njegere,dagaa,karanga na kadhalika.Ingawa unga wowote huweza tengeneza uji imezoeleka kwa wengi kwamba uji hupikwa kwa unga wa nafaka ambao wanga ndio kirutubisho kikuu ndani yake.
Kwakua unga wa vitu mbalimbali hubeba virutubisho aina tofauti tofauti,ni sawa kabisa kuchanganya unga aina tofauti tofauti ili kutengeneza unga mmoja ulioshehena virutubisho.
Miaka hii ya karibuni unga wa lishe umekua na jina kubwa sana,wajasiriamali wengi na viwanda vingi husindika na kufungasha unga wa lishe.Unga huu hutengenezwa kwa kuchanganya unga wa nafaka na unga wa vyakula  vingine  ili kuupa virutubisho vinavyohitajika katika lishe bora.Unga huu huuitwa lishe kwani kwa mtoto mdogo uji upikwao kwa unga huo ndio chakula chake kikuu,kwa maana nyingine huesabika kama chakula na si kinywaji.
Ingawa unga wa lishe umejaa madukani,ni vyema ukatengeneza unga wa lishe wewe mwenyewe ili kuhakikish mtoto anapatakilichobora.Wafungashaji wengi wa unga wa lishe wamekua ki biashara zaidi,kwani Ingridients(mahitaji yaliyotumika kuandaa unga huo) walizoandika juu ya mifuko si mahitaji kamili yaliyotumika kuandaa unga huo Na matokeo yake ni kufanya mteja anunue kisicho bora.Wengiwataandika karanga,soya na dagaa kama ingridients lakini hawaweki hata tone ,na wakati mwingine wanaweka katika uwiano usiokua sahihi.
Unga wa lishe wa MOUNT JOY ni unga safi kwa watoto ,nasema hivi kwani  nimeona unga huo ukiboresha afya za watoto wa dada na kaka zangu.Uji wa unga huo ni mtamu mdomoni,hata mtoto anakosa sababu ya kukataa uji.Unga huo hupatikana katika ujazo wa kilo moja, kwenye maduka na supermarkets mbalimbali jijini Dar es salaama .Kama kawaida yangu,sisifii chakula adi nikitie mdomoni na kuthibitisha  ubora wake.
Mtoto hujua chakula kizuri na kibaya,na wanapokua wadogo hawajaanza kuongea wao hufanya mambo kwavitendo.Mtoto anapokataa uji kila siku,badala ya kumkaba (kama muitavyo kina mama)jaribu kumbadilishia unga au uandaaji wa uji wake.Wakati mwingine mtoto anapokataa uji au chakula ni namna yake ya kukwambia chakula ni kibaya au hakipendi,hata ivyo kuna sababu nyingine nyingine zinazoweza fanya mtoto akatae chakula.
Watu wengi huwapa watoto uji na chakula bila kujali uzuri /ladha ya uji huo mdomoni kwa mtoto.Ukiandaa chakula chenye virutubisho vya kutosha alafu kikawa na ladha mbaya,basi juhudi zako hazina maana kwani mtoto hatakula chakula hicho.Ni vyema ukaonja chakula cha mtoto kabla hujampa endapo wewe hutapenda ladha yake basi ujue hata mtoto anauwezekano mkubwa wa kutoipenda.
Unapoandaa uji wa mtoto zingatia uzito wake kutokana na  umri wa mtoto.mtoto wa miezi 7 na mtoto wa mwaka moja uji wao hutofautiana uzito,hii ni kutokana na uhitaji wa mwili wa mtoto.Kiasi cha uji unachompa mtoto pia hutofautiana kutokana na umri pamoja na uzito wa mtoto.
Onyo.
Si kila unga wa lishe ni sawa au salama kwa mtoto yoyote.Wataalam wa afya wanashauri usichanganye zaidi ya aina mbili za unga unapoandaa unga wa mtoto chini ya mwaka mmoja,kwani uwezo wa mwili wa mtoto kumeng’enya chakula ni mdogo.Kwa upande mwingine ni ili kurahisisha kugundua chanzo cha tatizo endapo unga huo utamletea mtoto tatizo la tumbo au aleji ya aina yoyote.
Epuka unga wenye Soya  kwa mtoto chini ya miaka miwili,tafiti zinaonyesha kua asilimia kubwa ya watoto miili yao hukataa soya na matokeo yake wanapata aleji  za aina mbalimbali.Tatizo si kwamba soya ni mbaya bali ni uandaaji mbaya wa soya.(siku za usoni,tutajifunza kuhusu soya.)
Kwa wiki mbili sasa,nimekua  full time mama wa watoto wa dada yangu,Benjamin mwenye umri wa  miaka sita na Yared mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi nane,baada ya heka heka za maisha kuwalazimu wazazi wao kua nje ya mkoa.Na hivi ndivyo ninavyoaandaa uji wa watoto hawa.
Mahitaji
Unga wa lishe wa MOUNT JOY
Maziwa fresh
Blue band
Sukari
Maji kidogo tu kwa akili ya kukorogea unga
Njia
1.Weka maziwa fresh kwenye sufuria kisha bandika jikoni yachemke(hakikisha umechuja maziwa)
001
2.Katika kibakuli,weka unga wa lishe wa MOUNT JOY,kisha ongeza maji kiasi koroga na uchanganye vizuri,hakikisha ni laini bila mabonge
002
005
3.Katika sufuria la maziwa yaliyochemka ongeza mchanganyiko wa unga na maji,koroga mfululizo ili uji usitengeneze  mabonge.
007
009
010
4.Acha uji uchemke kwa muda mrefu kiasi ili nafaka na protini nzito iive.kisha ongeza blue band,koroga ili kuchanganya,ivisha tena kwa muda kidogo na uji utakua tayari.
011
5.Epua uji jikoni,mimina kwenye bakuli acha upoe kidogo kabla hujaongeza sukari.ukiweka sukari kwenye uji wamoto sana ndipo upooze,uji  utakatika na kua majimaji.mpaka hapo uji uko tayari kwa mtoto kunnywa.
014
015
Maelezo ya  ziada.
Matumizi ya maziwa badala ya maji katika uandaaji wa uji huu ni ili kuhakikisha  mtoto anapata virutubisho vyakutosha kutoka kwenye maziwa.Na kwasababu hapendi kunywa maziwa fresh basi sina budi kufidia kiasi cha maziwa anachotakiwa kunywa kwa kumuwekea kwenye chakula kingine na kuhakikisha kwamba mwisho wa siku amepata maziwa yakutosha. katika makala zilizopita nimeelezea umuhim wa maziwa na vyakula vitokanavyo na maziwa, Maziwa ni tajiri wa virutubisho.
Nimetumia blue band  na siku zote nashauri blu band kwenye chakula cha watoto kwasababu blue band inamkusanyiko wa inavirutubisho vingi kwa pamooja,ina vitamin A,D,E,B6 na B 12.
Ukipenda unaweza kuongeza kiini cha yai kwenye uji wa mtoto ili kuupa virutubisho zaidi.
Kumbuka kuzingatia wingi wa virutubisho muhim katika chakula cha mtoto siku zote.

Kinywaji uji ni uji usiokua na wingi wa virutubisho,mara nyingi huandaliwa kwa kuchanganya unga wa nafaka na maji.
Chakula uji  ni uji wenye virutubisho kwa mingi,mara nyingi huandaliw kwa kuchanganya unga wa lishe na maji,na huongezwa vionjo vingine(maziwa,blueband,kiini cha yai nakadhalika) ili kuupa virutubisho zaidi.
Mpe mwanao lishe bora si bora lishe.
CRD: TOLLYZ KITCHEN

1 comment:

Anonymous said...

simu yangu hiyo naomba mawasiliano nitapataje huo unga 0767537772 asante
\

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!