Sunday, 28 September 2014

CHAKULA BORA KWA MTOTO WA MIAKA MIWILI MPAKA MINNE: JINSI YA KUANDAA MTORI WENYE VIRUTUBISHO KWA MTOTO

047

Mtoto anaekula chakula bora huwa na afya bora na mwenyefuraha



Katika recepie hii ya mtori wa mtoto.Nimezingatia zaidi virutubisho vinavyoitajika ili kumpa mtoto kukua katika uwiano sahihi.“KWANINI MTOTO WAKO HAKUI KATIKA UWIANO ULIO SAHIHI”
Mahitaji
Ndizi bukoba 4 kubwa
Karoti kubwa  4
Nyanya kubwa 2
Vitunguu maji vikubwa 2
Hoho kubwa 2
Maji kikombe 1
Maziwa fresh vikombe vitatu
Blue band  kijiko 1 cha chakula kilichojaa vizuri
Chumvi robo kijiko cha chai
Njia
1.Osha Mboga zote vizuri kwa kutumia maji yanayochuruzika.Menya ndizi karoti,na vitunguu.kata hoho katikati na utoe mbegu.kisha kata kata vyote katika vipande vidogo na uviweke katika mabakuli tofauti.
2.Chukua sufuria,hakikisha sufuria ni kubwa ili kuacha nafasi inayotosha kwa ajili ya povu la maziwa yanapochemka.Katika sufuria anza kwa kuweka ndizi,alafu weka vitunguu,vikifuatiwa na nyanya.
035
3.Juu ya Nyanya weka hoho na kisha weka karoti.Chukua kikombe kimoja cha maji na uongeze kwenye mboga hizo alafu bandika jikoni,Hakikisha umefunika sufuria na ufuniko vizuri na hakuna nafasi ya kutoa hewa au mvuke kwenye sufuria.Usitumie moto mkali sana ili uzipe mboga hizo nafasi ya kutoa maji yake ya asili ambayo yamebeba virutubisho.
043
045
  • Lengo la kufunika sufuria na kutoacha nafasi ya kutoa mvuke ndani ya sufuria ni kulinda virutubisho visipotee,kumbuka kuwa baadhi ya virutubisho hupotea unapoacha sufuria wazi.
4.Maji yakielekea kuisha (usiache zikakauka kabisa)ongeza vikombe vitatu vya maziwa fresh ambayo hayajatolewa cream,kisha weka chumvi  na uache vichemke

050
5.Maziwa yakichemka na kuanza kupandisha povu juu tumia mwiko kukata povu kwa kulikoroga,acha yachemke kwa muda na uhakikishe ndizi na mboga zimeiva kisha ongeza kijiko kimoja cha blue band.
051
  • Maziwa yanatakiwa kuchemka na kuivia ndani ya mboga,ila usiache maziwa yakapungua sana.Vinatakiwa kua na sura kama hii katika picha.
6.vikiwa tayari,zima jiko na kisha geuze chakula hicho,kumbuka tu kwamba tangu mwanza chakula hikiakigeuzwi.lengo ni kuepusha chakula kuganda chini ya sufuria na kuungua,ndizi,nyanya na maziwa vina sifa ya kuungulia chini kwa haraka sana.
055
7.Epua chakula jikoni,acha kipoe au kipoeze kwa kutumbukiza sufuria la chakula ndani ya maji baridi.Kikipoa,tumia mashine ya kusaga matunda/blender au food processer  kusaga chakula ili kupata mtori mzito.Maziwa uliyotumia kupika yanaosha kabisa kusaga chakula hiki,huitaji kuongeza maji wala maziwa wakati wakusaga.
054
8.Pima kiasi unachotaka kumpa mtoto,kipashe moto ,pooza na umlishe mtoto.Kile kilichobaki,weka kwenye chombo chenye ufuniko,lisha funika na uweke kwenye frize.Kitoe na uyeyushe pale unapoitaji kukitumia.
060
  • Lengo la kuweka chakula kilichobaki ndani ya friza ni kuhakikisha kiko salama kwani chakula kinapoganda hakitoi nafazi kwa vijidudu vyovyote kukua ndani yake.Tafadhali sana usiweke kwenye friji.nasisitiza weka kwenye friza.
Maelezo ya ziada
Ingawa mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba tayari anaweza kula chakula cha kawaida na ijulikane si watoto wote huwa na uwezo huo katika umri huo.watoto wengine huchelewa  kuweza kula chakula kigumu.
Ata kama mtoto tayari anao uwezo wa kula chakula kigumu,ni vyema ukampa  aina hii ya chakula ili kukamilisha vile virutubisho anavyoitaji .Mtoto katika umri huu bado anaitaji uangalizi rasmi wa chakula chake.wakati wa chakula cha familia muache ale  chakula wanachokula wengine,na daadae ale chakula rasmi kwake.Mtoto katika umri huu anatakiwa kuwa na milo mikuu minne kwa siku na milo midogo miwili.Katika hii kilo mikuu minne,hakikisha milo miwili ni milo rasmi kwa ajili yake na hiyo miwili mingine ale na wanafamilia wengine.

1 comment:

Anonymous said...

Asanteh sana kipenzi hataivyo mwanangu anamiaka miwili sasa lakini hatakikula chochote anaonjaonja tu anajaza mdomoni hamezi

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!