Maafisa wanasema kuwa takriban watu 22 wameokolewa huku waokoaji wakiwatafuta watu zaidi.
Msemaji wa shirika la kukabiliana na majanga amesema kuwa zaidi ya watu millioni 2 nchini humo waliathiriwa na mafuriko hayo ambayo yalisababishwa na mvua kubwa.
Maafisa wanasema kuwa takriban watu 289 wamefariki katika mafuriko hayo nchini Pakistan kufikia sasa.
Zahid Ali mwenye umri wa miaka 27,mchumba wake Mashal pamoja na wageni walikuwa katika boti hiyo iliyokuwa ikielekea katika sherehe za kundeleza harusi yao.
Msemaji wa huduma ya uokozi katika eneo hilo la Punjab amesema kuwa familia hiyo ilionywa kuhusu mafuriko hayo.Maafisa wanasema kuwa boti hiyo iliojaa kupitia kiasi ilikuwa ikivuka mto Chenab uliofurika katikati ya mji wa Punjab eneo lililoathirika vibaya na mafuriko nchini Pakistan.
Bi harusi amesema kuwa alinusurika baada ya kushika mti wa stima.
Mazishi ya waathiriwa 17 yamefanyika huku waokoaji wakiendelea kuwatufuta wale waliotoweka.
VIA-BBC SWAHILI
1 comment:
aziz bilal22:15
1
Reply
Inalilaah wa inalilah rajiuni.
Post a Comment