Kampuni ya simu ya Airtel ikishirikiana na kituo cha runinga cha Trace na muimbaji wa Marekani mwenye asili ya Senegal, Akon wameanzisha shindano la kusaka vipaji vya kuimba barani Afrika.
Shindano hilo litafanyika kwenye nchi 13 ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda Zambia, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, The Democratic Republic of Congo (DRC) na Gabon.
Zawadi kwa mshindi wa shindano hilo ni mkataba wa kurekodi na label ya Akon, Kon Live, mkataba wa usambazaji kupitia Universal Music Group, na mafunzo ya muziki chini ya Akon yatakayofanyika Marekani.
Shindano hilo la miezi sita litaanza mapema October 2014.
No comments:
Post a Comment