Sunday, 10 August 2014

TOHARA KWA WANAUME INAPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VVU.

TAFITI kutoka nchi nyingi duniani zimebaini kwamba tohara kwa wanaume inapunguza maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa asilimia 60 kwa wanaume na asilimia 44 kwa wanawake.

Pia imebaini kwamba tiba ya ukimwi kwa mama mwenye VVU inapunguza maambukizi mapya kwa mtoto kwa asilimia 97 na tiba kwa watu wazima imepunguza kwa asilimia 96.
Hayo yamebainishwa juzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu wa Bunge, William Lukuvi ambaye alihudhuria mkutano wa 20 wa kimataifa wa Ukimwi uliofanyika Melbnurne, Australia.
Lukuvi alisema tafiti hizo zilibaini kwamba kuna makundi maalum ambayo maambukizi yako juu na yanaongezeka ikiwamo Tanzania.
“Serkali imejipanga kulifanyia utafiti eneo hili ili kupata idadi zaidi ya walioko kwenye makundi hatarishi pamoja na maeneo ambapo wanaweza kufikiwa na huduma za kinga na tiba”alisema Lukuvi.
Aliyataja makundi hayo kuwa wanaouza na kununua ngono, wafungwa, wavuvi, wanaofanya kazi kwenye machimbo, wanaojidunga sindano za dawa za kulevya, wanawake na wanaume wanaofanya ngono kinyume cha maumbile, wafanyabiashra na madereva wanaosafiri masafa marefu.
Mkutano huo ulioshirikisha nchi 146 na kuwakusanya wajumbezaidi ya 11000, ulibainisha kwamba watu walioambukizwa ukimwi wanafikia million 75 na kwamba maambukizi yamepungua katika nchi hizi kwa asilimia 33 ikiwamo Tanzania.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!