SERIKALI ya Sweden imetiliana saini mkataba wa sh. bilioni 11na Serikali ya Zanzibar kwa ajili ya kuisaidia miradi ya maendeleo ikiwemo nishati.
Mkataba huo ulisainiwa na Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha, Khamisi Mussa na afisa miradi ya maedeleo kutoka ubalozi wa Sweden, Malena Rosma jana mjini Vuga visiwani hapa.
Akizungumza baada ya hafla hiyo, Mussa alisema Sweden imekua nchi ambayo imekuwa ikisaidia Zanzibar katika miradi mbali mbali ikiwemo sekta ya nishati, elimu na miundombinu pamoja na shughuli za uchaguzi.
Alisema mradi huo wa nguvu za umeme utakua wa miaka minne na endelevu, lengo likiwa ni kuliwezesha Shirika la Umeme kufanya kazi kiufanisi.
Kwa mujibu wa Mussa, Zeco inategemea kutumia umeme mbadala badala ya kutumia ya ule unaotoka Tanzania bara kupitia cable za ndani ya bahari.
Aliishukuru serikali ya Sweden kwa misaada yao huku akisema kuwa anaamini nchi hiyo itaisadia Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao.
Naye, Afisa wa miradi ya maendeleo kutoka ubalozi wa Sweeden, Malena Rosma alisema lengo lao ni kuisadia Zeco ili iweze kufanya kazi zake kiufanisi kwa ajili ya kuiletea maendeleo Zanzibar.
Kwa upande wake, Katibu mkuu wa Zeco, Alhalili Mirza alisema fedha hizo zitatumika katika kupanga sera, kwani shirika halikwezi kuingia kuanza kutumia umeme mbadala bila ya kujipanga.
No comments:
Post a Comment