Ndege moja iliokuwa na abiria 40 imeanguka mjini Tehran nchini Iran.
Runinga ya taifa la Iran imesema kuwa abiria wote wamefariki .
Ndege hiyo inayojulikana kama Iran 141 ilitengezwa nchini Iran kupitia teknologia ya Ukraine.Ndege hiyo ya kampuni ya Taban Air imeripotiwa kuanguka katika makaazi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mehrabad Maghribi mwa mji wa Tehran.
Uchunguzi umeanzishwa kuhusu ni nini kilichosababisha ajali hiyo.
Iran imekabiliwa na ajali kama hizo katika siku za hivi karibuni kutokana na ndege zake zilizozeeka mbali na marekebisho mabaya inazozifanyia.
VIA-BBC
1 comment:
aziz bilal15:43
1
Reply
Lo technology ya kirussi ni noma sana ndege zao hazina uimara wowote ule
Post a Comment