Tumepata Habari kutoka kwa Muwakilishi wa Tanzania Diaspora kwenye Bunge La Katiba Mh Kadari Singo kwamba suala la Uraia Pacha linajadiliwa kwenye Kamati za Bunge la Katiba Kesho JUMATATU TAREHE 11/08/2014.
TUNAOMBA WOTE ambao mnaunga mkono suala hili kwa faida ya Tanzania na Vizazi vyake tutumie muda huu uliobaki kufanya Mawasiliano Binafsi na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba yeyote unayemfahamu ili kuwaomba walisapoti suala hili katika Kamati zao.
Ni muhimu vilevile kwa sisi wenyewe kutambua ni kwa nini tunaona Uraia Pacha utafaa kwa Tanzania. Kwani Tutakapojiuliza na kuelewa msimamo wetu sisi basi itakuwa rahisi kumuelewesha na mwingine.
WANA TANZANIA DIASPORA Waswahili tunasema "kilio na mwenyewe" hivyo kama ni msiba huu ni wa kwetu TZ Diaspora Community TUSHIKAMANE na TUSIMAME PAMOJA KUPIGANIA HILI KWA FAIDA YA NCHI YETU NA VIZAZI VIJAVYO.
Tafadhali wasiliana na Mjumbe yeyote wa Bunge Maalum La Katiba sasa hivi unayemfahamu ili uweze kujua msimamo wake na kuomba ushirikiano wake kesho kwenye majadiliano yao ya Kamati.
MUDA bado upo tuwasiliane na WaHeshimiwa Wabunge wa Bunge la Katiba pls....pls...
Asanteni.
1 comment:
aziz bilal03:16
1
Reply
Lo,hiyo ni habari moja njema sana kwani kulikuwa na utata mkubwa sana kwa sisi ambao tuna uraia wa nchi zingine.
Post a Comment