Wednesday, 6 August 2014

KESI YA GHOROFA YAAHIRISHWA

Jengo la ghorofa 16 lililoporomoka
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, jana imeahirisha kesi ya mauaji ya watu 27 kutokana na kuporomoka jengo la ghorofa 16, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime na wenzake 11 hadi Agosti 18.

Washitakiwa wengine ni mfanyabiashara, Razah Hussein Ladha, Godluck Mbaga, Wilbroad Mugabisyo, Ibrahim Kisoki, Mohamed Abdubakari, Charles Salu, Zonazea Anage, Vedasto Ferand, Michael Hemed  Hemed, Albert  Jones na Joseph  Ringo.
Mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, Mwendesha mashitaka, Bernard Kongora, alidai kuwa kesi hiyo imeahirishwa kutokana na upelelezi haujakamilika.
Washitakiwa hao wataendelea kubaki rumande kutokana na kesi inayowakabili kutokuwa na dhamana.
Wanakabiliwa na jumla ya makosa 24 ya kuua bila kukusudia kutokana na jengo la ghorofa 16 kuporomoka jijini Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, kesi inayomkabili Raia wa Kenya, Nelson Rading Onyango, anayekabiliwa na mashitaka saba likiwamo kosa la  kutoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila ya kuwa na leseni na kuisababishia hasara Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imeahirishwa.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Amina Kombakono, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiahirisha hadi Agosti 13, mwaka huu.
Mshitakiwa huyo anadaiwa kuisababishia hasara TCRA ya zaidi ya sh. bilioni sita.
VIA-TZ-DAIMA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!