Hali ni tete sana eneo la Mkolye, takribani km 4 toka Mjini Sikonge baada ya basi la Sabena toka Mbeya kwenda Mwanza na basi la A.M. toka Tabora kwenda Katavi kugongana uso kwa uso (head on collision).
Dreva wote wa mabasi hayo wamefariki hapo hapo, mmoja akiwa amekatika kichwa!
Nimeshuhudia abiria kadhaa wakiwa wamenasa ktk mabasi hayo, baadhi wakiwa wamekatika mikono na miguu!
Nitaweka picha muda si mrefu, lakini ni hatari saaaana ndugu zangu!
Abiria wapatao watano wamefariki hapo, na majeruhi zaidi ya 30 wamepelekwa ktk Hospitali ya Mission ya wilayani Sikonge.
================= Updates =================
Sorry, kazi ni kubwa kweli kweli! Robo tatu ya basi la Sabena imebonyea kwa kubamizwa na basi la A.M, nikimaanisha seat zote kuanzia kwa dreva hadi nyuma(3/4) kwishney!
Niko busy na ki-pick up changu tunasaidia kupeleka maiti na majeruhi hospital. Picha baadae wakuu. Ni hatari sana I see!
Picha za ajali
Hilo basi lenye mudguard inayosomeka 'zaidi' ni basi la Sabena, unaweza kuona lilivyokandamizwa karibu robo tatu!
Chanzo JMF.













1 comment:
aziz bilal05:06
1
Reply
madereva wa mabasi ya raia wengi wao ni walevi na wavutaji madawa ya kulevya kama vile bhangi na crack iwekwe sheria za kuwadhibiti mfano kupimwa kila week moja.
Post a Comment