Kufanya mazoezi kwenye ubao mpana (plank) ni moja ya mazoezi muhimu hasa ukilenga sehemu ya juu ya mwili wako.
Katika zoezi hili utatumia dakika 20 za mazoezi kwa namna sita tofauti — kumbuka kunyoosha mgongo na mikono yako kwa dakika kadhaa baada ya kumaliza mazoezi kwenye mbao hizo.
Maelekezo ya hatua hizo sita:
Plank Mountain Climbers: Ukiwa umenyoosha mikono kwenye ubao, kunja goti lako la kulia hadi kifuani, halafu badili miguu haraka goti lako la kushoto liwe kifuani na mguu uwe kwenye nafasi ya ubao. Wengine huwa wanatumia mipira maalum kushikilia. Fanya zoezi hili kwa dakika moja.



Elbow Plank With Donkey Kick: Anza ukiwa umejikunja viwiko kwenye ubao. Kunja goti lako la kulia na kubinua kisigino chako kuelekea darini kwa sekunde 30 kama unapiga farasi-teke, kisha badili miguu.



Plank Jumping Jacks: Katika staili hii, rusha miguu yako kwa kuitenganisha na kuirejesha pamoja. Fanya zoezi hili kwa dakika moja.





Up-Down Plank: Anza kwa kunyoosha mikono kwenye ubao. Shusha kiwiko chako cha kulia chini na kisha cha kushoto, ukikaribia kidogo kwenye ubao. Kisha nyoosha mkono wako wa kulia na baadaye wa kushoto, rudi kwenye hali ya kunyoosha mikono. Rudia kwa dakika moja.






Two-Point Plank: Anza kwa kunyoosha mikono, na tanua mkono wa kulia na mguu wa kushoto. Kunja goti na kiwiko chini ya mwili wako, na kisha nyoosha. Fanya hivi kwa sekunde 30 kila upande.















1 comment:
Alhaji Chambo11:04
1
we mrembo soph daah.
Post a Comment