Liberia imetangaza hatua za dharula dhidi ya ugonjwa wa Ebola kufuatia kasi kubwa ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Rais wa Liberia Hellen Sirleaf amesema nchi yake kwa sasa inakabiliwa na tatizo la ugonjwa huo huku baadhi ya wananchi wakiwa na uelewa mdogo kuhusiana na hatua za kujikinga na ugonjwa huo.
Hatua hiyo ya Liberia inakuja huku wataalamu wa afya toka shirika la afya Ulimwenguni WHO wakikutana Geneva, Switzerland, kujadili mbinu za kukabiliana na ugonjwa huo.Amesema baadhi ya shughuli za kijamii zimeahirishwa kwa muda ili kuepusha uwezekano wa watu kuambikizwa virusi vya Ebola.
Katika mkutano huo wa siku mbili wataalamu hao watajadili wautangaze ugonjwa wa Ebola kuwa janga la kidunia.
Baadhi ya wataalamu wa afya wanasema Liberia ianweza kuwa na hali mbaya zaidi kutokana na umasikini na uelewa mdogo wa raioa wa nchi hiyo.
Marekani na mataifa ya ulaya imesema kuwa inatafuta mbinu za pamoja katika kutokomeza ugonjwa huo.
Ugonjwa wa Ebola kwa nchi umebainika kuwepo Guinea, Sierra Leone na Nigeria ambapo zaidi ya watu 930 wamekufa kutokana na ugonjwa huo.
Saudi Arabian pia iimesema raia wan chi hiyo aliyebainika kuwa na virusi vya Ebola alivyovipata Sieerra Leone amekufa katika hospitali ya Jeddah ambapo anakuwa mgonjwa wa kwanza kufa nje ya Afrika.
No comments:
Post a Comment