Sunday, 27 July 2014

WENYE HALI DUNI DAR ES SALAAM WAONGEZEKA-MAJJID MJENGWA



Wenye hali duni Dar es Salaam wanaongezeka...
Ndugu, 
Kwenye moja ya mitaa ya Masaki alasiri ya leo, nimekutana na makundi ya watu wengi wao ni akina mama na watoto.



 Nilipodadisi nikaambiwa wanamsubiri tajiri maarufu Tanzania awape msaada wa sikukuu. Ni picha ya kuhuzunisha kwa kweli.
Bila shaka ni matokeo ya Watanzania wengi na hususan vijana kukimbilia Dar es Salaam kwa matarajio ya maisha ya nafuu ilhali hata ajira zenyewe kwa sasa ni za shida. Na haiwezekani tukaendelea na hali hii ya wanyonge hawa kuishi kwa kutegemea kusubiri misaada ya matajiri nje ya makazi yao, na bila kufanya kazi. Kuna haja ya kufikiria njia za kuwavutia vijana kubaki mikoani na kwenye wilaya, hivyo, vijijini pia. Huko bado kuna fursa nyingi na nafuu ya maisha kupitia uzalishaji mali. Inawezekana.
Maggid Mjengwa

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!