''KIUKWELI JEZI HII IMEMPENDEZA CHUJI''.
Aliyekuwa kiungo wa Yanga SC, Athumani Iddi 'Chuji' akiwa katika mzoezi na timu ya Azam FC leo asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni Kocha wa JKT Ruvu, Fredy Felix Minziro, aliwapokea wachezaji, Athuman Iddi 'Chuji', Henry Jeseph na Shamte Ally, katika mazeoezi ya timu yake yanayofanyika kwenye Uwanja wa Malalakuwa Kawe na kufanya nao mazoezi, huku akiwa na matumaini ya kuwapata wachezaji hao katika msimu ujao wa Ligi Kuu.
Minziro, alikaririwa akisema kuwa wachezaji hao yupo nao katika mazoezi ya timu yake lakini hajazungumza nao chochote kuhusu kujiunga na timu yake na iwapo wao watakuwa tayari kufanya hivyo basi atafurahi na atawapokea kwa mikono miwili.
Wakati akisema hayo Chuji yeye alihudhuria mazoezi ya timu hiyo ya JKT Ruvu kwa siku moja tu na hajaonekana hadi leo alipoibukia katika mazoezi ya timu yaAzam Fc huko Chamazi.
Katika mazoezi ya Azam Fc, Chuji aliweza kuonyesha uwezo na kumvutia kocha wa Azam, Joseph Omog, ambaye amesema kwa sasa anahitaji kuwa na wachezaji wazoefu, ili kuendana na mikikimikiki ya Ligi na michuano ya Kimataifa.
Athumani Iddi ‘Chuji’ akijumuika na wachezaji wa Azam katika mazoezi leo asubuhi, katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment