Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba, Bw. Deus Kibamba akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika leo Julai 17, 2014 kuelezea msimamo wa
JUKWAA LA KATIBA juu ya mwenendo uliopita wa bunge hilo.
Kiongozi
wa Shule Kuu ya Sheria nchini Kenya, Profesa Patrick Lumumba
alisisitiza suala la wanasiasa kurudi bungeni na kuhakikisha katiba mpya
inapatikana.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Wajumbe wa JUKWAA LA KATIBA wakisisitiza jambo.
Picha na Cathert Kajuna
***********
Picha na Cathert Kajuna
***********
Na Hellen Kwavava, Dar es Salaam.
Ushauri
Umetolewa kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba kuwa na Mtazamo mpya
utakaoiletea nchi maslahi pindi watakaporudi bungeni katika mchakato
wakutafuta katiba mpya unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.
Hata
hivyo kundi la Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) limezidi kushauri
wakirudi bungeni na kuendelea na majadiliano kwa msingi wa rasimu ya
katiba.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam leo Julai 17, 2014 na mwenyekiti wa
Jukwaa la Katiba, Bw. Deus Kibamba ambapo ameeleza kwamba wabunge
wanatakiwa kuachana na mtazamo wa kisiasa pamoja na lugha zisizo na staa
kwenye bunge hilo kwani wanatakiwa kuzingatia uzalendo kwanza.
Aidha
Bw. Kibamba amesema kwamba licha ya muda kuwa mfupi kuelekea katika
uchaguzi wa mwaka 2015 wao wanapendekeza juhudi zaidi zifanyike ili
kukamilisha upatikanaji wa katiba hiyo.
Naye
Kiongozi wa shule kuu ya Sheria nchini Kenya Profesa Patrick Lumumba
amewasihi wanasiasa wa nchini kuhakikisha katiba inapatikana kutokana na
matakwa ya wananchi kwani nchini jirani zimekuwa zikiiga mambo mengi
kutoka huku.
Bunge Maalum la katiba linatajiwa kuanza tena Agosti 5, 2014 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment