Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakipata maelekezo kutoka kwa viongozi wa tume
Kushoto no Ruth Masham Mkurugenzi idara ya mawasiliano ya Tume ya Taifa ya uchaguzi, anayefuata ni Kamishina wa tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu Justice John Mkwawa
Na Mathias Canal, Kwanza Jamii-Iringa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza mchakato wa uboreshaji wa daftali la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration(BVR) umefanyika mkoani Iringa ambapo Tume hiyo imepewa jukumu la hilo kupitia ibara ya Mwaka 1977 na vifungu vya 11, 12, na 15 (5) vya sheria ya uchaguzi ya taifa sura ya 343 na kwa uchaguzi wa madiwani kupitia vifungu vya sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa, sura ya 292.
Ruth Masham ambaye ni Mkurugenzi idara ya mawasiliano ya Tume ya Taifa ya uchaguzi, alifafanua kuhusu kuanzishwa mifumo mingine inayofanya kazi pamoja na mfumo wa utunzaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa lengo la kuboresha zaidi mchakato mzima wa uchaguzi.
Mashamu mifumo hiyo ikiwa ni pamoja na Mfumo wa menejimenti ya wagombea (Candidate Management System) unaowezesha kuandaa karatasi za mfano wa kura, Mfumo wa kutangaza matokeo ya kura (Result Management System), Mfumo wa Maghala Logistiki (Warehouse Management System), Mfumo wa mawasiliano na matukio ( Communication and Incidency Management System), Mfumo wa habari za kijiografia (Geographical Information System) pamoja na Mfumo unaotumika kuwawezesha wapiga kura kutambua vituo vyao vya kupigia kura (Voter Ineraction System).
Aliongeza kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali zilizosababisha wadau mbalimbali wa uchaguzi kwa kuhoji usahihi wake na hivyo kutokuaminika kwa baadhi ya wadau, ambapo alisema changamoto hizo ni pamoja na Kuwepo kwa watu waliofariki katika daftari, majina ya wapiga kura kutokuonekana kwenye daftari siku ya kupiga kura wakati watu walijiandikisha na wana kadi zao za kupigia kura, kushindwa kurekebisha taarifa zao au kumhamisha endapo mpiga kura huyo amehamia sehemu nyingine, kuwepo kwa majina ya wapiga kura waliojiandikisha zaidi zaidi ya mara moja na ambao taarifa zao kama vile dolegumba kutochukuliwa kwa usahihi ili wakati wa uhakiki liweze kutofautishwa na wapiga kura wengine.
Alisema changamoto hizo pamoja na nyingine ndizo zimeisukuma Tume ya Taifa ya uchaguzi kufikiria kutumia teknolojia nyingine itakayosaidia kuondoa changamoto hizi.
Aidha alisema Tume ya taifa ya uchaguzi imeanzisha na kuvihakiki vituo vipya katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa, awali vituo viliishia ngazi ya kata hivyo kusababisha kuwa na vituo vichache na wengi wakilalamikia kuwa na vituo vichache na wengi wakilalamika kuwa viko mbali na baadhi wapiga kura.
Kwa upande wake Kamishina wa tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu Justice John Mkwawa alisema uamuzi wa kutumia BVR umefikiwa kutokana na changamoto zilizojitokeza katika matumizi ya Teknolojia ya ‘’Optical Mark Recognition’’ (OMR) yaliyosababisha kwa kiasi kikubwa daftari la kudumu la wapiga kura kuwa na kasoro zilizosababisha baadhi ya wadau wa uchaguzi kuhoji uhalali wake.
Hata hivyo alisema mategemeo makubwa ya tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa matumizi ya (BVR) yatapunguza au kuondoa kabisa matatizo yaliyomo kwenye daftari lililopo ikiwemo kuzuia mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja.
Amewataja watumishi ambao wanahitajika katika zoezi la uandikishaji ni pamoja na Maafisa Waratibu wa Uandikishaji wa Mkoa Regional Registration Coordinators (RRCs), Maafisa Waandikishaji Registration Officers ROs ambao kwa mujibu wa sheria ni Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi Assistant Registration Officers (AROs), Waandishi Wasaidizi katika vituo vya uandikishaji, Biomettric Kit Operators, Watumishi watakaofanya kazi za Logistiki na kusafirisha taarifa kutoka katika vituo vya uandikishaji hadi Zonal Data Center au Center Data Center (Makao makuu ya Tume), pamoja Watumishi watakaofanya kazi Processing Center.
Sambamba na hayo Mkwawa alisema kuwa uandikishaji wapiga kura una hatua nyingi, hatua ya awali ni ya kuandaa vifaa vitavyotumika katika zoezi zima la kuandikisha upya wapiga kura wote wenye sifa, hatua itakayofuata ni kutoa mafunzo kwa watendaji watakaohusika katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Aidha aliongeza kuwa zoezi hili ni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kwa ajili ya kura ya maoni ya katiba mpya, mpiga kura atatumia kitambulisho cha mpiga kura atakachopatiwa na tume baada ya kuandikishwa katika mfumo huu tu na si vinginevyo, pia vitambulisho viatatolewa katika uandikishaji na uboreshaji uliopita havitatumika tena
No comments:
Post a Comment