Monday, 14 July 2014
HII MARA YA NNE UJERUMANI KUTWAA KOMBE LA DUNIA
Ujerumani imetwaa Kombe la Dunia kwa mara ya nne, baada ya kuibwaga Argentina 1-0 katika fainali zilizomalizika hivi punde Rio de Jenariro, Brazil.
Mario Götze dakika ya 113
Washangiliaji waliomimika kwa maelfu kuangalia mechi hiyo ya aina yake walikuwa wakiishangilia Argentina, huku zaidi ya raia 100,000 wa Argentina wakiripotiwa kumiminika nchini Brazil kupitia mpakani na baharini, lakini hilo halikuwadumaza Wajerumani. Mario Götze ndiye aliyeweka kimiani goli la kwanza na la pekee katika dakika 113 na hivyo kuiandika nchi yake kwenye kitabu cha historia ya ushindi wa Kombe la Dunia. Kwa mara ya kwanza Ujerumani ilishinda Kombe hilo mwaka 1954, kisha 1974 na 1990, wakati huo bado ikiwa imegawika kati ya mashariki na magharibi. Ushindi wa mara hii ni wa kwanza tangu mashariki na magharibi kurudi tena kuwa taifa moja la Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.
Wajerumani wakishangilia ushindi.
Manuel Neuer kipa bora, Lionel Messi mchezaji bora
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment