MSHAMBULIAJI wa Ujerumani, Thomas Muller amesema kamwe hajawahi kufungwa na timu ambayo ndani yake yupo Lionel Messi na atapenda kuendeleza hilo wakati watakapokutana na Argentina katika mechi ya fainali ya kombe la dunia siku ya jumapili.
Muller amefurahia michuano ya mwaka huu ya kombe la dunia kwa kufunga magoli matano katika mechi tano alizocheza mpaka sasa na magoli kama hayo yalimfanya abebe kiatu cha dhahabu nchini Afrika kusini mwaka 2010.
Nyota huyo wa Bayern Munich alisema yeye na wachezaji wenzake watafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanatwaa kombe la dunia kwa mara ya kwanza ikiwa imepita miaka 24.
KWA HISANI YA FULLSHANGWE
No comments:
Post a Comment