Kampuni kubwa ya ndege nchini Nigeria ARIK Air imesitisha safari zote za ndege zinazoelekea Liberia na Sierra Leone kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola katika eneo hilo.
Taifa hilo limeviweka katika tahadhari viingilio vyake baada ya mtu mmoja kufariki kutokana na ugonjwa huo siku ya ijumaa mjini Lagos.
Zaidi ya watu 660 wamefariki kutokana na ugonjwa huo tangu mwezi february katika kile kinachoonekana kuwa maambukizi mabaya zaidi ya ugonjwa huo katika historia yake.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa Kampuni ya ndege ya Air Arik imesema kuwa hatua hiyo ni ya tahadhari.
Vilevile imeitaka serikali ya Nigeria kuzizuia ndege zote zinazotoka katika mataifa hayo mawili kuingiza abiria nchini humo.
Wakati huohuo serikali imebuni maeneo ya kuwatenga washukiwa wa ugonjwa wa ebola katika viwanja vyote vya ndege vya kimataifa.
Kuna hofu kuwa maradhi hayo yakizuka Lagoz kunaweza kutokea janga kubwa kwa kuwa mamilioni ya watu wanaishi katika mji huo katika mazingira duni na msongamano mkubwa.
Hadi sasa hakujatokea habari zo zote kuhusu aliyeangukizwa maradhi hayo hatari ya Ebola tangu mwanamume mmoja aliyetoka Liberia kufariki nchini Nigeria mnamo Ijumaa
No comments:
Post a Comment