Tuesday 1 July 2014

RAIS KIKWETE KUBARIKI MAONYESHO YA UTALII

RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kufungua maonyesho ya kimataifa ya utalii ya Swahili Tourism  Expo yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba Mosi hadi 4 mwaka huu.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema hayo mwishoni mwa wiki jijini hapa alipozindua tovuti ya taarifa za maonyesho hayo iitwayo Swahili Tourism Expo (STE).
Maonyesho hayo yatahusisha kampuni binafsi, taasisi za kiserikali ikiwemo Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), nchi zote za Afrika Mashariki na Sudani watashiriki.
“Jukumu la kuandaa maonyesho haya lipo chini ya TTB… ofisi yangu itachukua jukumu la kipekee kufuatilia mialiko iliyotumwa kwa nchi mbalimbali kuhakikisha zinashiriki,” alisema waziri Nyalandu.
Alisema hiyo ni fursa ya kuongeza biashara ya kitalii nchini ambapo baada ya hapo Tanzania itapokea watalii zaidi ya milioni mbili kwa kuwa maonesho hayo yataitangaza nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB, Balozi Charles Sanga alisema maonesho hayo ni chachu ya kukuza utalii wa ndani.
“Maonyesho kama haya ni maarufu katika nchi za wenzetu… yasaidia katika kukuza sekta ya utalii nasi tunaanza na litakuwa linafanyika kila mwaka,” alisema balozi Sanga.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!