Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai nchini (DCI), Issaya Mungulu, katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Arusha leo, Jumanne Julai 22, 2014 imedaiwa kuwa Julai 21, 2014 saa 20.00 usiku katika maeneo ya Sombetini, Jeshi hilo limewakamata Yusufu Ally (30) na mkewe Sumaiya Juma (19) wakiwa nyumbani kwao baada ya kupekuliwa walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono Saba (7), risasi sita za bunduki aina ya shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo na bisibisi moja.
Mungulu amenukuliwa na FikraPevu akisema kuwa Yusufu ni miongini mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote jijini Arusha na kuwa mahojiano juu ya mtuhumiwa bado yanaendelea dhidi yake.
Aidha, amesema uchunguzi wa shauri hilo pamoja na matukio mengine ya milipuko yanaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi mwa polisi na kuwakamata watakaobainika kuhusika na matukio hayo.
Mtuhumiwa mwingine wa milipuko nchini asakwa na Polisi
Hata hivyo, Jeshi hilo limesema linamtafuta, Yahya Hella (33) mkazi wa Mianzini mkoani humo, mwenyeji wa Chemchemu, Kondoa – Dodoma kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya ulipuaji mabomu nchini.
“Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazowezesha ukamatwaji wa mhalifu huyu na pia nipende kuwashukuru sana wananchi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa jeshi letu hapa nchini” alisema Mungulu.
Watuhumiwa wengine kufikishwa mahakamani
Amesema kufuatia tukio la mlipuko wa bomu Julai 7, 2014 saa 22.15 usiku katika mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini Arusha, ambapo watu wanane walijeruhiwa vibaya, Jeshi hilo limewakamata watuhumiwa 25 kwa uchunguzi na kuwa kati yao watu sita watafikishwa Mahakamani mapema iwezakanavyo.
Amewataja watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo kuwa ni pamoja na Shaaban Mmasa (26) ambaye ni mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo kwenye mgahawa huo, Athuman Mmasa (38) na Mohamed Nuru (30), wote walinzi katika Mgahawa wa Chinese uliopo eneo la Gymkhana jirani na eneo la tukio.
Wengine ni Sheikh Jaffar Lema (38) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Olturmet katika wilaya ya Arumeru, pia alikuwa Imam wa Msikiti wa AL-QUBA mjini Arusha ambaye ametambuliwa kama mmoja wa viongozi walioratibu matukio ya milipuko ya mabomu maeneo balimbali nchini, Abdul Salim (31), wakala wa Mabasi Stendi Arusha, na Said Temba (42), mfanyabiashara wa Arusha.
ReplyDeleteSosthea Sosthenes19:48
1
Reply
OMG... God help!!!