Pages

Sunday, 20 July 2014

NAFASI YA SHAMPOO KATIKA NYWELE"

Matumizi ya bidhaa mbalimbali yamekuwa yakifanyika kutokana na mazoea tu. Wakati mwingine imekuwa ni vigumu kwa mtumiaji husika kueleza, umuhimu au faida za bidhaa anayoitumia.
Vivyo hivyo kwa shampoo. Shampoo ni miongoni mwa vipodozi ambavyo vimekuwa vikitumiwa mara kwa mara, hususan na wanawake. Aina hii ya kipodozi hutofautishwa kutokana na viungo vinavyotumika katika utengenezaji wake.
Tofauti hizo zimekuwa zikisababisha kuwepo kwa viwango tofauti vya ubora kulingana na matakwa ya mtumiaji. Lakini kwa ujumla wake shampoo ina umuhimu mkubwa katika nywele. Ukiachilia mbali usafishaji wa nywele shampoo ni muhimu katika kuboresha afya ya ngozi ya kichwa. Pia hurahisisha ukuaji wa nywele na hivyo kuzifanya ziwe zenye na rutuba.
Kazi nyingine ya shampoo ni uondoaji wa seli zilizokufa katika ngozi ya kichwa, jambo linalochangia kutoka nafasi kwa tundu za hewa katika ngozi ya kichwa kupumua vyema, kitendo kinachochochea kuota haraka kwa nywele.
Si hivyo tu, matumizi ya shampoo, hasa zile zinazotokana na mimea, husaidia katika kuziepusha nywele kutokana na maradhi mbalimbali kama vile m’ba na mengine yanayosababishwa na bakteria.
Pamoja na kuwa wengi wetu hupendelea kutumia shampoo, kwa kupenda harufu. Kwa mujibu wa wataalamu, matumizi ya aina hiyo ni huhatarisha uhai wa ngozi ya kichwa na nywele kwa jumla. Hii inatokana na baadhi ya kemikali zinazotumika katika utengenezaji wa shampoo hususan zile za viwandani kuwa si salama. Kwani badala ya kurutubisha nywele kutoka na ukali wake husababisha nywele zikatike.
Matumizi ya shampoo zinazotengenezwa na asali, shubiri, mayai ni sahihi zaidi, kwani husaidia kwa kiasi kikubwa siyo tu kukuza nywele, bali kuziboresha na hivyo kuziondolea matatizo mbalimbali likiwamo la kukatika.
Ili kufanikiwa katika yote haya, unashauriwa kutotumia shampoo kwa mazoea na badala yake kuangalia viungo vilivyotumika katika utengenezaji .

No comments:

Post a Comment