Pages

Sunday, 20 July 2014

MWANAMUZIKI JULIANA KANYOMOZI APOTEZA MTOTO WAKE

Juliana-Kanyomozi2-post
Mwanamuziki maarufu wa nchini Uganda, Juliana Kanyomozi, leo asubuhi amempoteza mtoto wake mdogo wa kiume Keron baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Pumu. Kwa mujibu wa gazeti na New Vision Keron amefariki katika hospitali ya Aghakhan.


Kanyomozi
Ni wakati mgumu kwa mwanamuziki huyo mrembo kwakuwa amekuwa akimpenda sana mtoto wake wakati akithibitisha taarifa hizo.
New Vision imemnukuu Juliana akisema kuwa” Malaika wangu ametangulia kwa Mungu, kilichosambazwa awali ni uzushi. Amefariki leo saa 10:25 asubuhi hii, amekuwa mpambanaji mkubwa wa afya yake nawashukuru wote kwa maombi yenu nitajitahidi kujikaza, Mungu amlaze mahali pema Keron lala salama mwanangu hadi tutakapokutana tena.”
Juliana amewaomba mashabiki wake kumuombea mtoto wake huyo haswa katika kipindi hiki kigumu kwake.
Juliana amesema mtoto wake hakuwa katika hali nzuri baada ya kushambuliwa na ugonjwa wa Pumu uliomsababishia kupoteza maisha.

3 comments:



  1. aziz bilal12:39




    lo pole sana dada yangu kwa kupoteza mwanao.

    ReplyDelete
  2. Sosthea Sosthenes19:57


    1


    Daah...pole dada kazi ya Mungu haina makosa!!!

    ReplyDelete
  3. Sosthea Sosthenes19:57


    1


    Daah...pole dada kazi ya Mungu haina makosa!!!

    ReplyDelete