Pages

Monday, 28 July 2014

MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA MBARONI KWA KULAWITI WATOTO WATANO

Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtoto wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la sita kwa tuhuma nzito ya kuwalawiti wenzake watano kwa mpigo.

Tukio hilo la kusikitisha lilijiri katika Mtaa wa Twanga Pepeta Kijiji cha Fulwe-Dindili Kata ya Mikese Wilaya ya Morogoro Vijijini mkoani hapa ambapo dogo huyo alidaiwa kufanya tukio hilo ambalo ni gumzo kwa sasa huku raia wenye hasira kali wakitishia kumshushia kipigo denti huyo waliyempa jina la Babu Seya endapo ataachiwa na jeshi la polisi.
Mwanahabari wetu alifunga safari hadi kijijini hapo ambapo baadhi ya wananchi waliohojiwa walidai kwamba dogo huyo alikuwa akiwalawiti wenzake kwa kigezo cha kuwapanga kwenye mechi za mpira wa matambara.

lli kupata undani wa tukio hilo, mwanahabari wetu alifika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kukuta tayari jeshi la polisi lilifika limeshamkamata.

Mjumbe wa serikali ya mtaa huo wa Twanga Pepeta Kitwana Tupa alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanasubiri sheria ichukue mkondo wake baada ya kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Poul.

No comments:

Post a Comment