Thursday, 24 July 2014

MILIONI 390 WAUGUA DENGUE

Milioni 390 waugua dengue
IMEELEZWA kuwa watu milioni 390 huugua ugonjwa wa dengue huku 25,000 wakipoteza maisha kila mwaka duniani kutokana na ugonjwa huo.

Mtaalamu wa udhibiti na ufuatiliaji wa magonjwa, Dk. Geofrey Mchau, alibainisha hayo wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari za afya, kuhusu magonjwa ya milipuko, hususan dengue ambao hivi karibuni uliua watu 1,384 mkoani Dar es Salaam.
Alisema kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo, kinga zaidi inahitajika ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira safi, kufukia madimbwi ya maji, vifuu na mashimo katika sehemu mbalimbali, magome ya miti na maua pia.
Aliongeza kuwa ugonjwa wa dengue hauna tiba wala chanjo kwa sasa, bali mtu anayeugua hutibiwa magonjwa nyemelezi yanayosababishwa na virusi hivyo.
Mtaalam wa ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa, Dk. Vida Mbaga, alisema matukio ya ugonjwa huo barani Afrika yameanza kuongezeka tangu mwaka 1980.
Alisema kuna dalili kuu za ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na homa kali, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo au uchovu na kutokwa damu kwenye fizi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!