Shirika la afya duniani, limewaasa wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, kutumia dawa za kupunguza makali ya HIV hata ikiwa hawajaambukizwa HIV.
Shirika hilo linasema kuwa ikiwa wanaume hao watatumia dawa hizo za kuzuia maambukizi pamoja na kutumia Condom, huenda ikapunguza maambukizi ya HIV miongoni mwao kwa zaidi ya asilimian 20.
Kikundi hicho cha wanaume ndicho kilichoanza kuambukizwa HIV miaka 33 iliyopita.Msemaji wa shirika hilo, alisema kuwa kiwango cha maambukizi miongoni mwa wanaume wapenzi wa jinsia moja, watu wanaotumia madawa ya kulevya , wafungwa na makahaba imeongezeka.
Miaka ya zamani dunia ilipoanza kuchukua hatua dhidi ya maradhi ya ukimwi kutokana na picha zilizokuwa zinatisha za wagonjwa wa Ukimwi, ripoti ya shirika hilo inasema kizazi cha leo hakijali sana kuhusu ugonjwa huo hasa kwa sababu kuna dawa za kupunguza makali.
Kwa mujibu wa WHO, haali hii inatishia juhudi dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo.
Kizazi cha leo kinakabiliwa na hatari ya kuambukizwa HIV zaidi ya maradufu. Mfano nchini Bangkok, idadi ya wanaoishi na virusi vya HIV kwa wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, ni 5.7%.
Katika mapendekezo yake mapya , shirika hilo linataka wanaume waanze kutumia dawa za kupunguza makali ya HIV kama njia ya kujikinga kutokana na maambukiz
VIA-BBC
No comments:
Post a Comment