NAIBU WAZIRI wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mhe. Juma Nkamia amemuomba mmiliki wa kiwanja cha michezo cha Azam Complex Bw. Said Salim Bakhresa kutoa ruhusa kwa wachezaji wa Tanzania kufanya mazoezi katika uwanja huo hasa wakati wa usiku ili ziweze kuwa katika nafasi nzuri na zipate uzoefu wa kucheza muda huo.
Hayo yamesemwa leo na Mhe. Nkamia katika kikao cha kukabidhiwa cheki na Bw. Bakhresa yenye thamani ya Dola 93,000 ili kuisaidia timu ya Taifa ya riadha kufika Glasgow, Scotland pamoja na mahitaji mengine kama jezi na vifaa.
“Fedha hii itasaidia timu yetu yenye wachezaji 39 ,makocha, pamoja na walimu waliotoka China kuweza kurudi salama.” Alisema Nkamia.
Aidha, Mhe. Nkamia ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuweza kuzungumza na wachezaji hao na kuwakabidhi bendera ya Taifa huko waendako.
Bw. Bakhresa amesema kuwa anaisapoti timu ya Taifa kwenda Scotland kwa sababu michezo siyo mpira wa miguu tu na amefafanua kuwa mashindano ya michezo ni kitu muhimu katika nchi na kinaleta maendeleo.
“Tunachokipata kinatokana na jasho la watanzania na tunakirudisha kwa watanzania,Tanzania inajengwa na watanzania wenyewe siyo watu wa nje”. Alisema Bakhresa.
No comments:
Post a Comment