Kamishna wa umoja wa mataifa anayehusika na haki za binadamu Bi Navi Pillay amesema kuna uwezekano mkubwa kuwa Israel imetenda uhalifu wa kivita wakati ikiishambulia Gaza.
Pillay ameyazungumza hayo kwenye kikao cha dharura cha baraza la umoja wa mataifa wa kitengo hicho cha haki za binadamu.
Bi Pillay ameelezea kutilia kwake shaka madai ya Israel kwamba ilifanya jitihada za kujaribu kuwaepusha raia wa Palestina na mashambulizi yake ya mizinga na ya majeshi ya ardhini huko Gaza waliosema lengo lao ni kuisambaratisha uwezo wa Hamas kuishambulia .
Bi Pillay ametoa mfano wa kisa cha kutamausha ambacho kilikiuka sheria za kimataifa ambacho watoto saba walileengwa na kuawa kutokana na mashambulizi hayo ya Israel walipokuwa ufuoni mwa Gaza.
Pia amelaani kitendo cha Hamas cha kuirusha makombora Israel.
Mwakilishi wa Israeli katika kikao hicho alisisitiza kuwa Israel inahaki ya kujilinda.
Waziri wa maswala ya haki wa Israili Tzipi Livni alisema kuwanchi yake inajua kuwa kitengo hicho Umoja wa mataifa kinaionea Israili na kuwa kinaipendelea Palestina.
Zaidi ya-Palestina 649 wameuawa katika mashambulizi hayo ya Israel ya wiki mbili za zilizopita, wengi wao wakiwa raia.
Waiisrael 31 nao wamefariki.Hayo yanajiri huku Israili ikiendelea na mashambulizi katika maeneo ya Kusini mwa Ukanda wa Gaza katika vitongoji vya Khan Younis.
Walioshuhudia wanasema kuwa takriban wapalestina 5,000 wamekuwa wakipeperusha vibendera vyeupe ilikuepuka mashambulizi ya Israili.
No comments:
Post a Comment